• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Waislamu wakerwa na hatua ya mahakama kuwapa mashoga uhuru wa kujisajili

Waislamu wakerwa na hatua ya mahakama kuwapa mashoga uhuru wa kujisajili

NA CECIL ODONGO

VIONGOZI na wasomi wa dini ya Kiislamu wamelaani vikali uamuzi wa Mahakama ya Juu kuruhusu makundi ya mashoga na wasagaji kusajiliwa.

Wakihutubu katika Msikiti wa Jamia, Mashekhe na wasomi walisema uamuzi huo utasababisha Waislamu na Wakenya kupoteza imani na utendakazi wa korti hiyo.

Naibu Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamia, Sheikh Abdullatif Essajee na msomi wa dini Sheikh Ahmadnur Mohamed waliongoza waumini kulaani uamuzi wa korti hiyo wakisema, unaenda kinyume na imani na hata tamaduni za jamii mbalimbali nchini.

Sheikh Essajee alisema kuwa uamuzi huo hata unaenda kinyume na Katiba ya Kenya ambayo inapendekeza kifungo cha hadi miaka 14 kwa mashoga na wasagaji. Alisifu mataifa jirani ya Uganda na Tanzania kwa kusimama wima na kukataa kuruhusu makundi hayo huko licha ya shinikizo za baadhi ya mataifa ya kigeni.

“Inashangaza ni kwa msingi gani majaji hao walitoa uamuzi huo. Kama Waislamu tunapinga uamuzi huo,” akasema Sheikh Essanjee.

Miaka 10 iliyopita, Bodi ya Kushirikisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali, ilikataa kusajili makundi ya mashoga kwa msingi kuwa yanaendeleza mapenzi ya jinsia moja.

“Ni wazi kuwa kuna shinikizo za kuendeleza tabia za ushoga nchini kutoka kwa mataifa ya nje. Tunamuomba Rais William Ruto achukue msimamo wa kuharamisha hili jinsi walivyofanya wenzake Yoweri Museveni na Samia Suluhu,” akaongeza.

Sheikh Mohamed naye alisema, ushoga na usagaji hata umepingwa na dini za Uislamu na Ukristo kwa hivyo, uamuzi kuwa tabia hiyo imeruhusiwa hata umemshangaza yeye. Aliongeza kuwa tendo la ndoa limeruhisiwa kati ya watu ambao wameoana na lazima tu iwe ni mume na mke.

  • Tags

You can share this post!

Pasta ageuka mgonganishaji wa waliopoteza mpendwa wao

Mwanamume adai yeye ni yatima anayehitaji kuwa na watoto...

T L