• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Wakenya waliokuwa na maringo sasa waegemea unga wa ‘kisiagi’

Wakenya waliokuwa na maringo sasa waegemea unga wa ‘kisiagi’

NA BARNABAS BII

WASAGAJI nchini wanakadiria hasara kutokana na kupungua kwa mauzo ya unga wa mahindi wa pakiti, baada ya wateja wengi kuegemea aina tofauti ya chakula kutokana na kupanda kwa bei ya unga na bidhaa nyingine za matumizi ya msingi.

Wakenya wengi ambao awali walikuwa na maringo, sasa wameamua kutumia unga wa mahindi wa ‘kisiagi’ badala ya ule wa pakiti, kwani bei yake ni ya chini, ikilinganishwa na wa pakiti.

Ni hali ambayo imeathiri sana mauzo ya wasagaji.

“Huwa ninanunua kilo mbili za mahindi kwa Sh100 na kuzisaga kwa Sh20. Gharama hiyo ni ya chini sana kuliko kununua unga wa pakiti,” akasema Bi Jane Kosgei, kutoka eneo la Saos, Kaunti ya Nandi.

Pakiti ya kilo mbili za unga wa mahindi inauzwa kwa kati ya Sh165 na Sh195 katika maduka mengi ya jumla katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Wakulima wengi wanataja bei hizo kuwa za juu sana, ikizingatiwa kuwa huu ni msimu wa mavuno. Pia, kuna mahindi ambayo yamekuwa yakiingizwa nchini kutoka mataifa ya Tanzania na Uganda.

Bei za mahindi zimeshuka kutoka Sh6,200 hadi Sh3,600 kwa miezi miwili iliyopita, hali ambayo imekuwa afueni kwa Wakenya wengi.

  • Tags

You can share this post!

Familia yaomba msaada wa serikali kumpata mfanyabiashara...

Videge wapendanao wageuza hoteli jukwaa la kulumbana

T L