• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Wanaume Murang’a hutandikwa sana na wake wao – Utafiti

Wanaume Murang’a hutandikwa sana na wake wao – Utafiti

NA MWANGI MUIRURI 

WANAUME wa Kaunti ya Murang’a ndio wanaongoza nchini kwa kuchapwa na wake wao, takwimu za utafiti zinaonyesha.

Kikundi cha utafiti kuhusu dhuluma za kijinsia pamoja na afya husika katika safu ya mapenzi (LVCT) kimefichua matokeo ya utafiti huo.

Mkurugenzi wa LVCT Bw Joshua Nyolo akihutubu katika Kaunti ya Murang’a mnamo Agosti 27, 2023, alisema kwamba kati ya wanaume 100 wa Murang’a, 11 hutandikwa na wake.

Wale wa Turkana nao wakiwa kwa kundi la 100, tisa hupigwa ngumi, makofi, mateke na hata kuchunwa na wake wao.

Wanaume wa Lamu huwa wanapigwa katika asilimia nane huku wa Kiambu wakitandikwa kwa asilimia sita sambamba na wale wa Tharaka Nithi.

Wale wa Isiolo hutandikwa kwa kiwango cha asilimia tano.

Kwa ujumla, wanaume nchini huchapwa na wanawake, Bw Nyolo akasema, lakini huwa wananyamaza ili wasiaibike au kutengwa.

“Wanaume wana kasumba kwamba hawafai kupigwa na wake na wakiwezwa na watandikwe, waiweke hiyo kuwa siri kubwa,” akasema.

Bw Nyolo aliwataka wanaume waanze kukataa kukaa kimya wakati wanaumia na kutandikwa na wake wao.

Wametakiwa pia wazingatie lishe bora, wafanye mazoezi na kuachana na uraibu ambao huwadhoofisha kiasi cha kuwa wepesi wa kuchapwa.

  • Tags

You can share this post!

Maoni mseto kuhusu sare mpya za polisi baadhi wakitaka...

Mwanamume ataka arudishiwe mkono wake uliokatwa miaka 16...

T L