• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 6:30 PM
Mwanamume ataka arudishiwe mkono wake uliokatwa miaka 16 iliyopita

Mwanamume ataka arudishiwe mkono wake uliokatwa miaka 16 iliyopita

KNA na KALUME KAZUNGU

MWANAMUME ameomba msaada kurudishiwa mkono wake uliokatika na kuhifadhiwa mochari miaka 16 iliyopita, akidai umekuwa ukimtembelea kwa ndoto ukitaka kuzikwa kiheshima.

Bw David Sanguli, 45, kutoka Mwatate, Taita Taveta, alisema mkono huo uliokatika kwa mashine katika shamba la mkonge ulihifadhiwa mochari Wesu, akashindwa kuuchukua kwa sababu ya deni la Sh106,000.

Waziri wa Afya katika Kaunti, Bw Gifton Mkaya, alisema hakuna rekodi za kuthibitisha madai hayo. Alisema alishashughulikia malalamishi hayo mwaka wa 2013.

“Kunayo sehemu ya mwili wangu inayopumzika katika mochari huku sehemu nyingine nikiwa nazo hapa. Ninataka sehemu hiyo inayokosekana irudishwe ili izikwe ipasavyo.”

Wakati huo huo, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), imebainisha kuwa watu 569 waliokuwa wamejumuishwa kwenye orodha ya wavuvi waliofaa kulipwa fidia Lamu, hawakustahili kulipwa.

Fidia hizo za jumla ya Sh1.76 bilioni zilifaa kutolewa na serikali kwa wavuvi ambao waliathirika na shughuli za ujenzi wa Bandari ya Lamu (LAPSSET).

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na EACC, imebainika pia kuwa majina 136 yalikuwa ni ya watu ambao hawapo. Vilevile, EACC ilitambua wavuvi halali 433 ambao walikuwa wameachwa nje ya orodha hiyo ilhali walifaa kufidiwa.

Mnamo Aprili 30, 2018, Mahakama Kuu mjini Malindi iliagiza serikali iwalipe fidia wavuvi 4,734.

Shughuli hiyo iliyokuwa tayari imeanzishwa, ilisimamishwa baadaye, EACC ilipoamuru hivyo ili orodha ichunguzwe. EACC ilichukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamishi kutoka kwa umma kwamba shughuli hiyo inafanywa isivyofaa.

  • Tags

You can share this post!

Wanaume Murang’a hutandikwa sana na wake wao –...

SHINA LA UHAI: Hatari, tija za mwanamke kujifungua akiwa na...

T L