• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Wandayi, Cherargei wakorogana kuhusu utendakazi wa polisi

Wandayi, Cherargei wakorogana kuhusu utendakazi wa polisi

NA WANDERI KAMAU

MOJA ya matukio yaliyogonga vichwa vya habari wiki hii, ni kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa mrengo wa Azimio la Umoja na polisi.

Baadhi ya viongozi waliokamatwa ni wabunge Babu Owino (Embakasi Mashariki), Ken Chonga (Kilifi Kusini), Spika wa Kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire na madiwani kadhaa.

Ijapokuwa baadhi ya viongozi walikamatwa na hatimaye kuachiliwa, hali ilikuwa tofauti kwa Bw Owino, kwani mara tu baada ya kukamatwa na polisi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA), Jumanne usiku, alisafirishwa moja kwa moja hadi katika Kituo cha Polisi cha Wang’uru, kilicho katika Kaunti ya Kirinyaga katika hali tatanishi.

Ni hatua iliyozua ghadhabu kali miongoni mwa wafuasi wa Azimio, baadhi yao akiwemo Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Opiyo Wandayi, aliyedai kuwa ni kinyume kwa polisi kumzuilia mtu kwa zaidi ya saa 24 bila kumfikisha mahakamani.

Hata hivyo, Seneta Samson Cherargei (Nandi) aliwapongeza polisi kwa ‘kufanya kazi nzuri’.

Opiyo Wandayi-Kiongozi wa Wengi, Bungeni alisema: “Chini ya Katiba ya 2010, ni kosa polisi kumzuilia Mkenya yeyote; bila kujali hadhi au nafasi yake katika jamii, zaidi ya saa 24 bila kumwambia sababu ya kukamatwa au kuzuiliwa bila kumfikisha mahakamani. Huo ni ukiukaji mkubwa wa Katiba!”

Naye Samson Cherargei Seneta wa Nandi alisema: “Polisi walifanya kazi yao vizuri. Sijui ni kwa nini wanalaumiwa. Hii ni ishara tumewashinda Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kwenye juhudi zao za kuivuruga nchi.”

 

  • Tags

You can share this post!

Uhuru alivyofaulu kukwepa ‘mtego’ wa polisi Karen

Gavana Kang’ata alaumiwa kwa kukubalia mabaa kupigia...

T L