• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Zubeidah Kananu achaguliwa kuwa rais wa Baraza la Wahariri nchini

Zubeidah Kananu achaguliwa kuwa rais wa Baraza la Wahariri nchini

Na WINNIE ONYANDO

MHARIRI wa KTN Zubeidah Kananu ndiye rais mpya wa Baraza la Wahariri Nchini (KEG).

Bi Kananu alipata kura 73 dhidi ya mpinzani wake wa pekee Sammy Muraya wa Journalists for Human Rights aliyepata kura 36 kwenye uchaguzi uliofanywa Nairobi Club jana.

Msimamizi wa uchaguzi huo Wakili Tom Onyango pia aliwatangaza; Ruth Nesoba wa BBC kuwa naibu rais, Francis Mureithi wa The Star (kuwakilisha mtandao), Linda Bach wa Standard Group (magazeti), Millicent Awuor na Toepista Nabusoba wa KBC kuwakilisha televisheni na Redio mtawalia, profesa George Nyabuga wa Chuo Kikuu cha Aga Khan (vyuo vya uanahabari).

Nao Arthur Okwemba na Martin Masai walichaguliwa tena katika bodi ya wasimamizi.

Uchaguzi huo ulifanywa baada ya marekebisho ya katiba ya KEG yaliyoweka vikwazo vya mihula. Churchill Otieno aliyeongoza mihula miwili alistaafu rasmi.

 

  • Tags

You can share this post!

Msaada kwa walioathirika na mafuriko Nakuru

Vijana wa Homa Bay, Makueni watawala soka ya kaunti

T L