• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 1:01 PM
9 wauawa katika vita Somaliland

9 wauawa katika vita Somaliland

NA MASHIRIKA

BOSASO, SOMALIA

MAPIGANO makali yaliendelea kwa siku ya tisa mfululizo katika eneo la Somaliland, Jumamosi, huku watu tisa wakiuawa.

Eneo hilo ni miongoni mwa maeneo machache ambayo yametangaza kujitenga na Somalia na kujitangazia uhuru.

Kulingana na afisa mmoja wa ngazi za juu wa serikali, mapigano hayo yaliendelea licha ya serikali ya eneo hilo kuagiza mashambulio hayo kukomeshwa mara moja.

Somaliland ilijitenga na Somalia mnamo 1991, ijapokuwa haijapata utambuzi kimataifa kuhusu uhuru wake.

Serikali ya eneo hilo imekuwa ikikumbwa na upinzani mkali katika maeneo ya Las Anod na maeneo yaliyo karibu, ambako baadhi ya viongozi wa kiukoo wanataka eneo hilo kujiunga na Somalia. Viongozi hao wamekuwa wakivilaumu vikosi vya Somaliland kwa kushindwa kukabili hali ya ukosefu wa usalama.

“Vikosi vya Somaliland vinashambulia maeneo ya raia kwa kutumia roketi na silaha nyingine hatari,” akasema Abdurahim Alui Ismail, ambaye ni meya wa Las Anod, kwenye mahojiano na wanahabari.

“Daktari aliyekuwa akiwatibu watu waliojeruhiwa kwenye mapigano hayo ameuliwa serikalini.”

Viongozi wa Somaliland hawakutoa taarifa mara moja kuhusiana na kauli hizo.

Wizara ya Usalama wa Ndani nchini humo ilisema kuwa vikosi vyake vilikuwa vikijilinda baada ya kushambuliwa na ‘wanamgambo’, huku ikisisitiza kuwa vikosi hivyo vitaendea kudumisha mwafaka wa kusitisha amani uliotangazwa Ijumaa.

“Serikali ya Somaliland inatangaza kuwa vikosi vyake havikuwa vikitekeleza mashambulio, bali walikuwa wakijilinda,” ikaeleza serikali kwenye taarifa.

Mapigano katika eneo la Las Anod, ambao ndio mji mkuu wa eneo hilo, yalianza baada ya kamati ya viongozi wa eneo hilo, wasomi wa kidini na mashirika ya kutetea haki za umma kusema Jumapili iliyopita kwamba hawalitambui eneo hilo kama taifa huru. Walisisitiza kuwa wanataka kujiunga na Somalia.

Kwenye mapigano yaliyozuka Jumatatu na Jumanne, jumla ya watu 58 waliuawa.

Mnamo Jumanne, jumla ya watu 24 waliuawa huku 53 wakijeruhiwa, kulingana na ripoti zilizotolewa na madaktari.

Viongozi wa kiukoo wanaotaka eneo hilo kujiunga na Somalia wanashikilia uongozi wa eneo hilo umeshindwa kukabili changamoto zinazoikumba.

Kwenye vita vilivyotokea Jumanne, wapiganaji kutoka eneo jirani la Puntland, ambalo pia limejitangazia uhuru, walidaiwa kushirikiana na wanamgambo kuvikabili vikosi vya Somaliland, jambo ambalo eneo hilo limekanusha.

Madaktari walisema kuwa miili ya watu 58 ilipelekwa katika hospitali mbalimbali mjini Las Anod baada ya mapigano hayo kuanza. Walisema imekuwa vigumu kwa watu wengi waliojeruhiwa kufika hospitalini kutokana na mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea.

Viongozi walisema kuwa huduma muhimu kama maji na umeme zimekatizwa kutokana na mashambulio hayo.

  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Serikali iendelee kutatua changamoto...

Chai ya muasumini na manufaa yake kwa binadamu

T L