• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Bola Tinubu wa chama tawala APC achaguliwa kuiongoza Nigeria

Bola Tinubu wa chama tawala APC achaguliwa kuiongoza Nigeria

AFP Na MOHAMMED MOMOH

LAGOS, NIGERIA

CHAMA tawala nchini Nigeria cha All Progressives Congress (APC) kitasalia mamlakani baada ya mgombea wake wa urais Bola Tinubu, 70, kutangazwa mshindi na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC) leo Jumatano.

Tinubu amezoa kura 8.8 milioni dhidi ya 6.9 milioni za mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP) Atiku Abubakar ambaye alikuwa makamu wa rais wa zamani.

Mgombea wa chama cha Leba Peter Obi, naye alikuwa wa tatu kwa kuzoa kura 6.1 milioni.

INEC imesema Tinubu alipata kura 8,805,428 akifuatwa na Abubakar aliyepata kura 6,984,520 huku Obi naye akipata kura 6,093,962 kufunga tatu bora. Mgombea mwingine, Rabiu Kwankwaso wa New Nigeria People’s Party (NNPP) amepata kura 1,496,671.

Vyama vya upinzani havijaridhishwa na matokeo, baadhi ya viongozi wao wakisema yalichakachuliwa kumpa mgombea wa serikali ushindi.

“Huu uchaguzi umechakachuliwa pakubwa,” alisema mwenyekiti wa chama cha Leba Julius Abure mnamo Jumanne akitaka uchaguzi huo ufutwe.

  • Tags

You can share this post!

Gharama ya maisha yakeketa raia – Ripoti

TAHARIRI: Serikali itilie mkazo elimu ya wanafunzi wa Gredi...

T L