• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Buhari ateua mabalozi waliojiuzulu kuwa mabalozi

Buhari ateua mabalozi waliojiuzulu kuwa mabalozi

Na Mashirika

ABUJA, Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amewateua makamanda wanne wakuu wa jeshi waliojiuzulu wiki jana kuwa mabalozi.

Rais huyo alibadilisha wakuu wa jeshi huku miito ikizidi afanye mabadiliko kutokana na ukosefu wa usalama kote nchini humo.

Alikubali kujiuzulu kwa mkuu wa majeshi na makamanda wakuu wa jeshi la nchi kavu, majini na angani na akaidhinisha kustaafu kwao kutoka huduma za kijeshi.

Mnamo Alhamisi, aliwasilisha majina yao kwa seneti waidhinishwe kuwa mabalozi wa nchi tofauti. Duru zilisema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa seneti itaidhinisha uteuzi wao.

Nigeria imekuwa iking’ang’ana kukabili kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likifanya mashambulizi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kuteka nyara watu wakiwemo wanafunzi wa shule.

Visa vya ujangili pia vimekuwa vikishuhudiwa kote nchini humo.

Rais Buhari pia aliongeza muda wa kuhudumu wa inspekta jenerali wa polisi kwa miezi mitatu zaidi.

You can share this post!

Adhabu ya kadi nyekundu dhidi ya David Luiz wa Arsenal...

Mbio za Nyika za Pwani kufanyika Wundanyi Jumamosi