• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 4:54 PM
Canada yazima ndege za Urusi katika anga yake

Canada yazima ndege za Urusi katika anga yake

Na AFP

OTTAWA, Canada

CANADA imezuia ndege zote za Urusi kutumia anga yake kama hatua ya kuonyesha kukerwa na hatua ya nchi hiyo kushambulia Ukraine, serikali ya Canada ilisema Jumapili, Februari 27.

“Tutaiadhibu Urusi kwa kushambulia Ukraine bila sababu yoyote maalum,” waziri wa Uchukuzi Omar Alghabra akasema kupitia Twitter.

Hatua ya Canada kufunga anga zake kwa ndege za Urusi, iliyoanza kutekelezwa mara moja, inaenda sambamba na hatua ambazo mataifa mengine ya bara Uropa.

Hata hivyo, hakujakuwa na safari za ndege za moja kwa moja katika ya viwanja vya ndege vya Canada na Urusi.

Lakini hatua hii ya Canada itaathiri safari za ndege za Urusi kwa jina Aeroflot kuelekea na kutoka Amerika na mataifa mengine ya kusini.

Ndege yoyote inayomilikiwa, kukodishwa au kutumiwa na rais wa Urusi—zikiwemo zile za kibinafsi sasa ni marufuku kutumia anga ya Canada, msemaji wa Wizara ya Uchukuzi Valerie Glazer akiambia AFP kwa njia ya barua.

Mataifa mengine ya Uropa ambayo yamefunga anga zao kwa ndege za Urusi kupinga hatua yake ya kuvamia Ukraine ni Ujerumani, Ufaransa, Italia, Ubelgiji, Austria, Uholanzi na Uswisi.

Uingereza ilizuia ndege ya Urusi kwa jina Aeroflot mnamo Alhamisi.

Mnamo Jumapili, Februari 27, 2022, hakuna ndege kutoka Urusi zilizowasili katika viwanja vikubwa vya ndege nchini Amerika katika majimbo ya Washington, Baltimore, New York, Los Angeles na Chicago.

Shirika la ndege la Delta, Ijumaa lilisitisha kwa muda ushirikiano wake na Aeroflot.

Lakini Wizara ya Uchukuzi nchini Amerika haijatangaza hatua ya kupiga marufuku ndege za Urusi katika anga ya nchi hiyo.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Wakulima wa kahawa wahimizwa kuchukua mikopo isiyotozwa riba

Kocha Bielsa afutwa kazi baada ya Spurs kuponda Leeds 4-0

T L