• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Hunter amweka babake Rais Biden wa Amerika pabaya kwa tuhuma za uhalifu

Hunter amweka babake Rais Biden wa Amerika pabaya kwa tuhuma za uhalifu

NA MASHIRIKA

MWANAWE Rais wa Amerika Joe Biden, Hunter Biden, Alhamisi alifunguliwa mashtaka ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria.

Hunter anatuhumiwa kwa kusema uongo kuhusu matumizi yake ya dawa za kulevya aliponunua bunduki mnamo Oktoba 2018, kipindi ambacho alikiri kukabiliwa na uraibu wa kokeni.

Mashtaka hayo dhidi ya Hunter, 53 yamezua mjadala mpya kwenye kampeni za babake ambaye pia anamezea mate kiti cha urais.

Wakati huo huo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Alhamisi ilionya kwa mara nyingine kuhusu kutokea kwa mzozo wa kidiplomasia kati yake na nchi jirani ya Rwanda kutokana na uchokozi wake.

Haya yanajiri siku chache kabla ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoongozwa na Rais wa Baraza hilo Dennis Francis huko New York, unaolenga kustawisha uchumi wa nchi wanachama.

Wakihutubia wanahabari, Waziri wa Mawasiliano Patrick Muyaya na Waziri wa Sheria Rose Mutombo, walitoa malalamishi dhidi ya Kigali huku wakisema kuwa Rwanda imeanza tena uchochezi.

Wawili hao walisema kwamba Rwanda ambayo ni jirani wa Congo upande wa mashariki, inaunga mkono waasi wa Kitutsi wa M23, suala ambalo Rwanda imekuwa ikkana.

Waasi hao wamechukua udhibiti wa eneo kubwa kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini ulioko kwenye mpaka kati ya mataifa hayo, tangu 2021, baada ya miaka kadhaa ya utulivu.

Muyaya alisema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuna ukatili unaoendeshwa na jeshi la Rwanda likishirikiana na waasi wa M23.

Wataalam wa UN pia wamekuwa wakiilaumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao, wakati EU hapo Julai ikilalamikia kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Akiwasilisha taarifa ya waraka wa awali kuhusu suala hilo, Waziri Muyaya alisema mzozo huo umewalazimu zaidi ya watu milioni 2.3 kukimbia makazi yao.

Pia alisema kuwa kuna uharibifu mkubwa katika Mbuga ya Kitaifa ya Virunga ambayo itagharimu serikali ya nchi hiyo mamilioni kukarabati.

“Kutokana na mgogoro huo, watu walihama na kuyaacha makazi yao. Hii itaathiri pakubwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu,” akasema Muyaya.

Mwezi Agosti, Washington ilitangaza vikwazo dhidi ya watu sita, hasa viongozi wa waasi, ikisema kuwa watu hao wamechangia kuongezeka kwa mzozo mashariki mwa DR Congo.

Mnamo Januari, serikali ya DR Congo ilishutumu Rwanda kwa kutumia suala la wakimbizi kulipiza kisasi.

Hayo yalijiri baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kutangaza kuwa nchi hiyo haitabeba mzigo wa kuwapokea wakimbizi wa DRC Congo.

Novemba 2022, Umoja wa Mataifa ulisema takriban wakimbizi 72,000 wa Congo walivuka na kuingia nchini Rwanda.

Kundi hilo lilianza vita tena mwishoni mwa 2021 kwa sababu ya kile walidai ni hatua ya serikali ya DRC kudinda kutimiza ahadi ya 2013.

Wapiganaji wa kundi hilo wametekeleza mashambulio matatu makubwa mashariki mwa DRC tangu Machi 2022.

Katika shambulio walilotekeleza mwanzoni mwa Oktoba 2022, mamia ya watu walikufa na wengine zaidi ya 200,000 kutoroka makazi yao.

  • Tags

You can share this post!

Silambi matapishi, Pique amjibu Shakira zogo la mapenzi...

Man-City waendea ‘Nyundo’

T L