• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Pigo kwa Tedros Ethiopia ‘ikimkataa’ kwa madai ya kuunga waasi

Pigo kwa Tedros Ethiopia ‘ikimkataa’ kwa madai ya kuunga waasi

Na AGGREY MUTAMBO

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus amepata pigo, baada ya Ethiopia kusema kuwa haitamuunga mkono kuwania kiti hicho kwa muhula wa pili.

Ethiopia inadai kuwa Tedros amekuwa akiunga mkono waasi wa kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF), ambao wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo.

Tedros amewahi kuwa waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ethiopia kabla ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa WHO.

Wizara ya mashauri ya kigeni iliandikia barua Bodi ya Wakurugenzi ya WHO, ambapo ilisema kuwa Tedros atachafua sifa ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

“Amekuwa akiunga mkono kundi la waasi wa TPLF na kutatiza uhusiano baina ya Ethiopia na nchi jirani ya Eritrea,” ikasema Wizara ya Mashauri ya Kigeni.

Ethiopia inataka bodi ya WHO yenye wajumbe 34 imchunguze Tedros kwa ‘kushirikiana na waasi’.

Tedros ndiye mwaniaji wa pekee ambaye ameonyesha nia ya kuwania wadhifa huo katika uchaguzi utakaofanyika Mei.

Mnamo Oktoba, Kenya, Rwanda na Botswana ziliandikia bodi ya WHO ambapo zilielezea kumuunga mkono Tedros.

  • Tags

You can share this post!

OKA mahututi

Polisi wakamata 4 wanaoshukiwa kula na kuuza nyama ya...

T L