• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Polisi wakamata 4 wanaoshukiwa kula na kuuza nyama ya binadamu

Polisi wakamata 4 wanaoshukiwa kula na kuuza nyama ya binadamu

NA MASHIRIKA

ZAMFARA, NIGERIA

POLISI katika jimbo la Zamfara kaskazini-magharibi mwa Nigeria, jana Ijumaa walikamata watu wanne wanaodaiwa kula na kuuza nyama ya binadamu.

Kamishna wa polisi katika jimbo hilo, Elkanah Ayuba, alisema kuwa washukiwa hao walikamatwa baada ya maafisa wa upelelezi kupata maiti katika jengo ambalo halijakamilika huku baadhi ya sehemu za mwili zikiwa zimetolewa.

Ilikuwa ni katika harakati za kufanya uchunguzi wa kupotea kwa mvulana wa miaka tisa.

Kuhusika na uuzaji wa sehemu za binadamu na ulaji nyama si jambo la kawaida katika jimbo la Zamfara.

Lakini ni mojawapo ya maeneo ya Nigeria yaliyokumbwa zaidi na wimbi la mauaji na utekaji nyara kwa ajili ya fidia na magenge yenye silaha huku mamlaka zikikabiliwa na ukosoaji kwa kushindwa kukabiliana na ghasia hizo.

Kamishna huyo alisema vikosi vya usalama pia vimewaokoa watu 17 waliotekwa nyara katika jimbo jirani la Niger na kupelekwa Zamfara.

Alisema vikosi vya usalama vilivyokuwa kwenye doria pia vimefanikiwa kupata baadhi ya silaha ikiwa ni pamoja na vifaa vya kurusha roketi kutoka kwa genge moja baada ya makabiliano ya risasi karibu na msitu.

Wiki iliyopita, takriban watu 200 waliripotiwa kuuawa wakati wa msururu wa uvamizi katika vijiji kadhaa jimboni humo.

You can share this post!

Pigo kwa Tedros Ethiopia ‘ikimkataa’ kwa madai ya...

TUM kuanza kutoa mafunzo ya udaktari

T L