• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Tanzania yakana madai ya ulanguzi wa wanyamapori kutoka Serengeti hadi UAE

Tanzania yakana madai ya ulanguzi wa wanyamapori kutoka Serengeti hadi UAE

NA MASHIRIKA

DAR ES SALAM, TANZANIA

MAMLAKA ya safari za ndege nchini Tanzania (TCAA) imekana madai kuwa iliruhusu ulanguzi wa wanyamapori kutoka mbuga moja hadi mataifa ya Mashariki ya Kati.

Hii inafuatia madai kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanyamapori wanasafirishwa kwa ndege za mizigo kutoka Loliondo, karibu na mbuga maarufu ya kitaifa ya Serengeti hadi kwa Muungano wa Milki za Kiarabu (UAE).

Lakini TCAA imetaja madai hayo kama “ya uongo” ikisema uwanja wa ndege wa Loliondo si kituo cha kuingia na kuondoka nchini Tanzania.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Mwaka mmoja wa pata potea: Rais aanze kibarua sasa

Mpishi mwenye ulemavu wa macho atupwa jela miaka 30 kwa...

T L