• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:50 AM
Ushoga: World Bank yauma miradi ya umma Uganda

Ushoga: World Bank yauma miradi ya umma Uganda

NA AFP

KAMPALA, UGANDA

BENKI ya Dunia almaarufu World Bank mnamo Jumanne ilitangaza kwamba imesitisha kufadhili miradi ya umma nchini Uganda, baada ya taifa hilo la Afrika Mashariki kupitisha sheria ya kupinga ushoga na usagaji.

World Bank ilifikia uamuzi huo baada ya kushinikizwa na makundi ya kutetea haki za mashoga na wasagaji pamoja na Bunge la Marekani la Congress.

“Lengo letu ni kuyalinda makundi ya watu wachache wenye msimamo tofauti wa masuala ya mapenzi ambao huenda wakatengwa wasipate huduma na manufaa kutokana na miradi tunayofadhili,” World Bank ilisema kwenye taarifa.

Mnamo Julai 2023, wanachama kadhaa wa Congress walimtaka Rais wa World Bank Ajay Banga “kuahirisha mara moja na kusitisha ukopeshaji wa pesa sasa na siku zijazo kwa taifa la Uganda” hadi sheria hiyo ifutwe.

Ingawa hivyo, shirika hilo limesema linaendelea kuwasiliana na serikali ya Uganda inayoongozwa na Rais Yoweri Museveni.

  • Tags

You can share this post!

Azimio wamteua Kioni kuongoza timu ya ushauri wa kisheria

Ndoa za mitara zitatatua changamoto Mlimani – Wanguku

T L