• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
Wanamapinduzi Niger wadai wamezima jaribio la Rais Bazoum kutoroka jela akitumia helikopta

Wanamapinduzi Niger wadai wamezima jaribio la Rais Bazoum kutoroka jela akitumia helikopta

NA MASHIRIKA

NIAMEY, NIGER

WATAWALA wa kijeshi Niger walisema kuwa Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum, alijaribu kutoroka siku ya Alhamisi.

“Majira ya saa tatu asubuhi, rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum na familia yake, wapishi wake wawili na maafisa wawili wa usalama, walijaribu kutoroka kutoka katika kizuizi,” msemaji wa serikali Amadou Abdramane alisema kwenye televisheni ya taifa.
Kufuatia tukio hilo, wahusika wakuu waliopanga njama hiyo walikamatwa.

Kadhalika, Abdramane alisema kuwa uchunguzi umeanzishwa.

Rais huyo na familia yake walipanga kutumia helikopta kuelekea Nigeria.

Tangu alipopinduliwa na jeshi mnamo Julai 26, Bazoum amekataa kujiuzulu. Hadi sasa, alikuwa ameshikiliwa katika makazi yake katikati ya ikulu ya rais pamoja na mkewe Haziza na mwanawe Salem.

Mnamo Septemba, mawakili wa Bazoum walisema aliwasilisha kesi ya kisheria katika mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas) dhidi ya wale waliomwondoa madarakani.

ECOWAS imekuwa ikikashifu vikali mapinduzi hayo, kwa kuweka vikwazo kadhaa vya kiuchumi na usafiri kwa viongozi wa mapinduzi hayo. Pia, ilisimamisha utoaji umeme kwa Niger.

Pia mawakili hao wa rais huyo walisema wanapeleka kesi yake kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.

Maafisa wa jeshi waliopindua Bazoum walisema huenda rais huyo alitoroka kutokana na kuzorota kwa usalama wa nchi kufuatia mashambulizi ya wanamgambo.

Niger inapambana na waasi wawili wa wanamgambo: sehemu iliyoenea kusini mashariki mwa nchi hiyo kutoka kwa mzozo wa muda mrefu katika nchi jirani ya Nigeria; na mashambulizi katika magharibi ya wanamgambo wanaovuka kutoka Mali na Burkina Faso.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Niger ilifanya maombolezo ya kitaifa ya siku tatu baada ya wanajeshi 29 kuuawa katika shambulio linaloshukiwa kuwa la wanamgambo, ambalo ni baya zaidi tangu jeshi kuchukua mamlaka mwezi Julai.

  • Tags

You can share this post!

Kawira alijipandisha mwenyewe kwenye karandinga, Polisi...

Walioachiliwa kuhusiana na mauaji ya dereva wa teksi...

T L