• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
AFYA NA JAMII: Faida za kiafya za mafuta ya kungumanga

AFYA NA JAMII: Faida za kiafya za mafuta ya kungumanga

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KUNGUMANGA yaani nutmeg kwa Kiingereza, ni kiungo maarufu kinachopendwa sana na wapishi. Kiungo hiki hutumiwa kwa kiasi kidogo kutoa ladha tamu kwa chakula.

Mafuta ya kungumanga yenyewe yana faida kadhaa za kiafya. Mafuta haya muhimu yanayotokana na viungo hivi vyenye afya kupitia mchakato wa kunereka, na mchanganyiko huu ni muhimu sana katika kutibu magonjwa kadhaa.

Kungumanga huboresha mzunguko wa damu na oksijeni

Mafuta ya Nutmeg yana harufu tofauti ambayo husaidia katika matibabu ya wale wanaosumbuliwa na mzunguko mbaya wa damu. Matumizi ya mafuta ya kungumanga kwa namna yoyote huimarisha usafirishaji wa oksijeni kwa seli zote za mwili wako.

Huondoa mkazo na kupunguza uchungu

Mafuta ya kungumanga yanajulikana kusaidia kupambana na mafadhaiko, kwani hufanya kazi kama kichocheo na kitulizo. Yanaweza pia kusaidia kupunguza shinikizo la damu wakati mwingine hivyo kuleta utulivu na kupunguza mafadhaiko. Mafuta haya hutumiwa katika dawa tofauti ili kupunguza uvimbe wa viungo na maumivu ya misuli. Pia yanajulikana kwa uwezo wake wa kupunguza maumivu.

Hupunguza maumivu ya hedhi

Ikiwa mtu anaugua maumivu ya tumbo, uchovu au kutokua na usawa wa homoni wakati wa siku za hedhi, mafuta ya kungumanga yanaweza yakasaidia kutuliza hali mbaya. Mafuta haya yanajulikana kuwa na virutubisho vinavyosaidia mchakato mzima wa hedhi na kudhibiti pia mzunguko wenyewe. Yana athari bora za masaji ya aromatherapy katika kupunguza maumivu.

Huboresha na kuleta usingizi

Yanapofanya kazi kama kitulizo cha kupunguzia mwili dhiki na kuondoa mfadhaiko, mafuta ya kungumanga yanasaidia katika kuleta usingizi kwa ufanisi na kuboresha ubora wa usingizi huo.

Husaidia usagaji bora wa chakula

Sio wengi wanaofahamu kuwa mafuta ya kungumanga yanasaida kwa mmeng’enyo wa chakula. Matatizo kama vile gesi tumboni yanaweza kusababisha kadhia nyingine kama vile kuumwa na tumbo, lakini habari njema ni kwamba mafuta haya husaidia kukabili matatizo hayo.

Huondoa harufu mbaya na maambukizi ya kinywa

Mafuta haya ambayo hutumiwa kama manukato ya asili, yanaweza pia kusaidia kutibu tatizo la kudumu la harufu mbaya ya kinywa na magonjwa kadhaa yanayohusiana na mdomo na kinywa.

  • Tags

You can share this post!

LISHE: Umuhimu wa smoothies kwa afya ya binadamu

LISHE: Chakula chenye protini ya juu unachoweza kula kama...

T L