• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:50 AM
LISHE: Chakula chenye protini ya juu unachoweza kula kama kiamsha kinywa

LISHE: Chakula chenye protini ya juu unachoweza kula kama kiamsha kinywa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

BILA shaka kila mtu anajua kwamba kiamsha kinywa ni chakula muhimu zaidi.

Chakula cha staftahi kinaweza kukusaidia kuanza siku yako kwa njia ifaayo kwa kukupa nishati na kukufanya uwe mchangamfu.

Hayo kando, ni wachache tu kati yetu wanaozingatia ukweli huu. Kuruka kiamsha kinywa kunaweza kuonekana kuwa njia rahisi ya kuokoa wakati asubuhi, lakini kufanya hivyo mara kwa mara kunaweza kudhuru afya yako.

Unapoamka, mwili wako unahitaji madini na virutubisho ambavyo huongeza nishati kusaidia misuli yako na ambayo hutoka kwa kuvunja protini. Kwa hivyo, unahitaji kiamsha kinywa chenye protini nyingi ili kuupa mwili nguvu, kusaidia misuli yako, na kukufanya ushibe.

Ni muhimu pia kuongeza lishe yako na utaratibu wa kawaida wa mazoezi.

Mayai

Mayai ni chakula kimojawapo chenye virutubisho vingi vinavyopatikana kwani ni chanzo bora cha madini, vitamini, mafuta yenye afya na antioxidants. Vile vile mayai ni yana protini muhimu.

Mayai yaliyochemshwa. PICHA | MARGARET MAINA

Dengu

Dengu ni chanzo kikubwa cha protini inayotokana na mimea. Dengu ni nafaka za jamii ya kunde zenye nyuzinyuzi nyingi. Pia huwa na madini ya manganesi, chuma na folate ambazo ni nzuri kwa afya yako.

Kuku

Ulaji wa kuku unakupa hakikisho la kupata protini bora. Ni rahisi kupika kuku na hulika katika sahani mbalimbali. Kwa mfano, unaweza kuongeza kwa saladi, supu na koroga. Pamoja na protini, kuku hutoa aina mbalimbali za vitamini B na madini kama zinki na seleniumu.

Maharagwe

Maharagwe yana kiwango cha juu cha protini. Unaweza kupika maharagwe kwa njia mbalimbali, kama vile kuongeza kwenye supu na saladi.

Pia yana wanga tata, chuma, folate, nyuzi, fosforasi, manganese, potasiamu, na misombo ya mmea yenye faida. Zaidi ya hayo, chakula kilicho na maharagwe na mboga nyingine kinaweza kusaidia kupunguza lehemu. Kwa kuongeza, husaidia kupunguza shinikizo la damu na kudhibiti kiwango cha sukari ya damu.

Samaki

Samaki huwa na protini nyingi, vitamini na madini mengi ambayo ni pamoja na iodini, seleniumu, na vitamini B12. Zaidi ya hayo, samaki huwa na mafuta mengi ya Omega-3. Bila shaka chakula hiki kina faida nyingi za afya, ikiwa ni pamoja na kusaidia afya ya moyo.

  • Tags

You can share this post!

AFYA NA JAMII: Faida za kiafya za mafuta ya kungumanga

Mudavadi: Kufanyia kazi ‘kijijini’ kutanipa fursa...

T L