• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Boresha afya: Haya ni baadhi ya matumizi mengi ya ndizi

Boresha afya: Haya ni baadhi ya matumizi mengi ya ndizi

NA PAULINE ONGAJI

KWA watu wengi picha ya ndizi iliyoiva kupindukia haipendezi, na tunda hili linapoonekana hivi kwa wengi suluhisho huwa kulitupa pasipo kujua kwamba bado kuna manufaa ya kiafya kutokana na chakula hiki.

Ndizi mbivu huimarisha mfumo wa mmengényo wa chakula na pia zina viwango vya juu vya nyuzi. Aidha, chakula hiki kina kiwango cha chini cha kalori, kumaanisha kwamba kinasaidia katika harakati za kupunguza uzani.

Kuna mbinu za mapishi ambazo unaweza kutumia kuandaa ndizi badala ya kuzitupa:

Mkate

Unapoandaa mkate waweza kutumia ndizi badala ya sukari. Kumbuka kuwa jinsi ndizi hizo zinavyoonekana kuwa nyeusi na kuiva kupita kiasi, ndivyo zinavyozidi kufaa katika maandalizi ya chakula hiki kwani kitakoleza ladha zaidi.

Smoothies and milkshakes

Ndizi zinapoiva na kuonekana kupondeka ndivyo zinavyoonekana kufaa katika maandalizi ya smoothie na milkshake. Ladha yake ya kipekee pamoja na wepesi wake vinafanya ndizi kufaa katika maandalizi ya vyakula hivi.

Pancakes

Kata ndizi zilizoiva kupita kiasi kwa silesi kweye pancakes zako kisha uzikorooge na kuzipika. Hapa kiungo hiki chaweza kutumiwa badala ya sukari.

Biskuti

Changanya silesi za ndizi mbivu kupita kiasi kwenye mchanganyiko wa kinyuya cha biskuti kabla ya kukoroga na kuoka. Mbali na kuongeza ladha, kiungo hiki kitafanya biskuti zako kuwa nyepesi na tamu.

Oatmeal

Katakata silesi za ndizi mbivu kupita kiasi kisha uziponde kwa kutumia uma kabla ya kuzikoroga kwenye bakuli lako la shayiri. Kadhalika, hapa unaweza kuongeza mdalasini kuongeza ladha.

Jemu

Unapochanganya ndizi mbivu kupita kiasi pamoja na sukari na kuziacha kwa muda, basi upata jemu yako ya kupaka kwenye mkate.

Aiskrimu

Weka ndizi zako kwenye friza kisha baadaye uzipinde na kuziongeza kwenye aiskrimukama mbinu ya kuongeza ladha na harufu ya kupendeza kwenye chakula chako.

  • Tags

You can share this post!

Barabara mbovu: Mvua kubwa ilivyotatiza usafirishaji wa...

Wawili wanaswa kufuatia mkasa wa kufa maji kwa watahiniwa...

T L