• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 AM
JIJUE DADA: Mwasho ukeni baada ya kushiriki tendo la ndoa

JIJUE DADA: Mwasho ukeni baada ya kushiriki tendo la ndoa

Na PAULINE ONGAJI

WANAWAKE wengi hukumbwa na mwasho ukeni siku kadhaa baada ya kushiriki tendo la ndoa na kukumbwa na wasi wasi.

Kuna sababu kadha wa kadha ambazo husababisha haya. Kwanza, huenda mwasho huu unatokana na ukavu katika sehemu hii au msuguano mwingi. Ikiwa basi hii ndio sababu, basi mwasho utatokomea baada ya siku kadhaa ikiwa utaepuka tendo la ndoa.

Ikiwa mwasho utaendelea, huenda tatizo hili linatokana na ukavu katika sehemu ya uke, shida ambayo yaweza sababishwa na kukaukiwa kutokana na matumizi ya dawa za kihomoni, kwa sababu ya maradhi ya kisukari, au matumizi ya sabuni zilizo na harufu kali.

Pia, huenda hii ikatokana na mzio wa aina fulani ya kondomu au mafuta ya kulainisha uke wakati wa tendo la ndoa. Mwasho pia waweza kuwa kutokana na maambukizi hasa iwapo utaambatana na harufu mbaya, au majimaji yasiyo ya kawaida.

Litakuwa jambo la busara kumuona daktari na ufanyiwe uchunguzi wa kimatibabu ili kubaini iwapo una maambukizi, na hivyo upate tiba. Ikiwa kuna maambukizi, mwenzako pia atalazimika kutibiwa ili kuzuia maambukizi mapya. Ikiwa uke wako haujalainika vilivyo au unakumbana na ukavu ukeni kutokanana sababu moja au nyingine, unaweza tumia mafuta ya kulainisha uke wakati wa tendo la ndoa.

You can share this post!

Familia yafurahia Krismasi baada ya miaka 32

Anapenda upishi, sasa ana kiwanda cha kupika pilipili

T L