• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Akothee: Mume wangu ni moto masuala ya mahaba

Akothee: Mume wangu ni moto masuala ya mahaba

Na SAMMY WAWERU

MWANAMUZIKI tajika Esther Akoth almaarufu Akothee amemmiminia sifa chungu nzima mumewe mpya katika masuala ya mahaba.

Akothee amemtaja Dennis Schweizer, kibarafu wake wa moyo kama gwiji katika kitanda.

Kitanda, anamaanisha haki ya mume au mke kwenye ndoa.

Mwimbaji huyo wa kibao maarufu cha Kula Ngoma, alifunga pingu za maisha majuzi na mchumba wake Dennis ambaye ni mzungu katika harusi ya kipekee iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi mashuhuri serikalini na wanasiasa tajika, pamoja na wasanii wenzake.

Mwanamuziki tajika Akothee asema mumewe ni gwiji masuala ya mahaba. Picha / HISANI

“Ana hulka zote ninazotaka kwenye mwanamume. Zaidi ya yote ni hodari katika masuala ya kitanda,” Akothee alielezea kupitia chapisho la Facebook Alhamisi, kwenye ukurasa wake rasmi.

Msanii huyo ambaye ni mama wa watano, alionekana kukerwa na wakosoaji wake wanaodai aliolewa na Dennis anayemtambua kwa jina la utani kama Omosh kwa sababu ya pesa.

Moto kitandani

Akionekana kulenga wanaume, Akothee alishangaa ni kwa nini wanazongwa na wivu kwa kuwa aliondoka soko la wanaosaka wachumba.

“Haha mume wangu anawapa wanaume siku kucha zisizo na usingizi. Siwezi nikaoa mtu tu hivyo, na endapo ingekuwa hivyo ningeoleka kitambo. Mimi ni moto na mrembo ajabu, hivyo basi ninavutia watu kama Omosh,” alisema.

“Siwezi nikaoleka kwa sababu ya utajiri, nina utajiri wangu na iwapo utajiri ungetumika kama mizani ya ndoa nilikataa posa tatu za bilionea. Mwanamke kama mimi ni nadra kupatikana. Nilioa mkuu na ninaelewa hadhi yake, pamoja na familia yake na utajiri wake,” alifafanua.

Akothee na mume wake Dennis Schweizer. Picha / HISANI

Wawili hao walifunga pingu za maisha mapema mwezi huu, Aprili 10 katika mkahawa wa kifahari wa Windsor, jijini Nairobi.

Waziri wa Masuala ya Jinsia, Aisha Jumwa, mbunge wa Mbita Millie Odhiambo na mwenzake wa Lang’ata Felix Oduor maarufu kama Jalango ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria.

Harusi nyingine inatarajiwa kufanyika Switzerland, anakotoka mume wake mzungu.

Iliyofanyika nchini Kenya, familia ya mchumba wake haikuonekana hasa wazazi wa Dennis Schweizer.

  • Tags

You can share this post!

Kipindupindu: Wafungwa wa gereza la Thika waendelea kupata...

Bernard Wanjohi Njathi: Mwanzilishi wa shirika la kusaidia...

T L