• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Amepania makubwa katika tasnia ya uigizaji

Amepania makubwa katika tasnia ya uigizaji

Na JOHN KIMWERE

WAHENGA hawakupaka mafuta kwenye mgongo wa chupa, waliposema kuwa penye nia pana njia, maana ndivyo ilivyo tangia zama hizo na ipo hivyo mpaka sasa.

Usemi huo umeonyesha mashiko ya haja miongoni mwa jamii. Aidha ni msemo unaozidi kudhihirishwa na wengi ambao wameamua kujituma kisabuni kwa kujiamini wanaweza kusudi watimize malengo yao maishani.

Pauline Kyalo ni kati ya waigizaji wa kike wanaoibukia hapa nchini. Anasisitiza kuwa amepania makubwa katika tasnia ya uigizaji. Kando na usanii dada huyu ni mwanasayansi wa mazingira ambapo amehitimu kwa shahada ya digrii kwenye Chuo Kikuu cha Kenyatta.

BETTER DAYS

Binti huyu aliyezaliwa mwaka 1995, ingawa alianza kushiriki masuala ya burudani tangia akisoma shule ya msingi safari yake ilianza rasmi akiwa mwanafunzi wa mwaka wa pili mnamo 2003. ”

Ninasema hivyo maana ndio tulitengeneza kipindi kiitwacho ‘Sunday School Academy’ kilichopata mpenyo na kupeperushwa kupitia KUTV,” alisema na kuongeza kuwa anajituma kiume anakolenga kuibuka mwigizaji wa kimataifa miaka ijayo. Alishiriki kipindi hicho akiwa na kundi la Sparks Theatre lililokuwa chini ya dairekta Derrick Waswa.

Kisura huyu anasema kando na kuwa tangia akiwa mtoto alidhamiria kuhitimu kuwa mwanasayansi ama wakili alivutiwa na uigizaji mwaka 2003 akiwa darasa la pili alipotazama kipindi cha Better Days ambacho Joyce Musoke alikuwa mhusika mkuu.

Pauline Kyalo msanii anayekuja katika masuala ya uigizaji. ..Picha/ JOHN KIMWERE

12 YEARS A SLAVE

Anajivunia kushiriki Crime and Justice (Showmax ) pia ‘MaEmpress’ (Maisha Magic na DSTV). Pia Necessary Madness, What cant kill You, Lwanda Rockman na Tom Mboya kati ya zingine. K

atika mpango mzima amefanya kazi na makundi kadhaa ikiwamo Hearts of Art, Chatterbox, Too Early for Birds na Sparks Theatre. Dada huyu anasema amepania kuiga wenzake waliobeba katika tasnia ya uigizaji kama Viola Davis mzawa wa Marekani pia Mkenya Lupita Nyong’o walioshiriki filamu kama Fences na 12 Years a Slave kati ya wengine.

Kwa waigizaji wa hapa nchini angependa sana kufanya kazi na Joyce Musoke pia Wakio Mzenge ambao wameshiriki ‘Crime and Justine’ na ‘Selina’ mtawalia. Ndani ya miaka mitano ijayo analenga kumaliza masomo ya masuala ya uigizaji na kushiriki filamu kadhaa za nguvu.

MAWAIDHA

Ingawa hajapiga hatua katika sekta ya uigizaji kamwe sio mchoyo wa mawaidha. Anahimiza wenzie kuwa endapo wanahisi wana kipaji hawapaswa kuvunjika moyo wala kukata tamaa baada ya kukosa nafasi mara kadhaa. ”

Jambo lingine ningependa kuwapa wenzangu ni kuwa wasiwe wepesi kupata umaarufu hasa kwa kukubali kuingia mahusiano ya kimapenzi na maprodusa ambao hupenda kuwashusha wanawake,” akasema.

kuwa serikali inastahili kuunga mkono sekta ya uigizaji kwani imekaa vizuri kutoa nafasi nyingi za ajira kama ilivyo katika mataifa yaliyotangulia ikiwamo Nigeria, Afrika Kusini bila kuweka katika kaburi la sahau taifa la Tanzania.

Pauline Kyalo msanii anayekuja katika masuala ya uigizaji….Picha/ JOHN KIMWERE

You can share this post!

PCPB yaendelea kunyoosha mjeledi kwa wahuni wa dawa bandia...

Kibra yizidi kupepea ligi ya daraja ya kwanza

T L