• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 3:09 PM
Amerika, NATO hawatamuweza Putin kwa sasa

Amerika, NATO hawatamuweza Putin kwa sasa

NA CHARLES WASONGA

VIKWAZO ambavyo Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakitekeleza dhidi ya Urusi ndani ya wiki moja iliyopita vitaathiri uchumi wa nchi hiyo, na mataifa ya ulimwengu lakini havitasitisha vita Ukraine haraka.

Wadadisi wanasema hii ni kwa sababu Urusi ina njia mbadala ya kuendesha uchumi wake licha ya kufungiwa nje katika mfumo wa kifedha, SWIFT, kupitia kufungwa kwa akaunti za benki kuu nchini humo, Sberbank.

“Licha ya kufungwa kwa akaunti ya benki kuu ya Urusi yenye dola 640 bilioni (Sh64 trilioni) katika hifadhi za kigeni za sarafu, nchi hiyo ingali na hifadhi ya dhahabu ya thamani ya dola 127 bilioni (Sh127 trilioni) na hifadhi ya madini ya renminbi ya thamani ya dola 70 bilioni,” Dkt Samuel Nyandemo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi alisema katika makala aliyoandika katika gazeti la The People Daily, Jumatano.

Hatua hiyo imedhoofisha thamani ya sarafu ya Urusi inayojulikana kama rouble, hali ambayo itaathiri sekta ya biashara nchini humo.

Kwa hivyo, kulingana mtaalamu huyo, Rais Vladimir Putin anaweza kuendelea “kukaa ngumu” na kuendeleza juhudi zake za kuangusha utawala wa Rais Volodymyr Zelensky japo kwa muda mfupi.

Watetezi wa Putin hata hivyo wanashikilia kuwa kiongozi huyo ana uwezo wa kuvumilia makali ya vikwazo hivyo kwa muda wa mwaka mmoja.

“Lakini ukweli ni kwamba vikwazo hivyo vitaathiri pakubwa uchumi wa Urusi na chumi za mataifa yanayoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nchi hiyo, kama vile Kenya,” Dkt Nyandemo, ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi akaongeza.

Kenya huagiza bidhaa kama vile ngano, mafuta ya kupitia, mbolea, malighafi ya kutengeneza mabati miongo – ni mwa bidhaa nyinginezo.

Vikwazo vya kibiashara vilivyowekewa Urusi bila shaka vitasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa hizi nchini Kenya na mataifa mengine.

Wiki jana, mataifa ya 43 ya magharibi yalizima ndege zote kutoka Urusi kupitia katika anga zao, hatua ambayo imeathiri uwezo wake kusafirisha bidhaa zake katika mataifa ya nje.

Wizara ya Biashara nchini imefunga uuzaji wa bidhaa za kiteknolojia kama vile kompyuta na malighafi ya kuten – geneza zana za kivita nchini Urusi kwa lengo la kulemaza jeshi lake.

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) pia yamezima uuzaji wa bidhaa mbalimbali kwa sekta za kawi, uchukuzi na teknolojia nchini Urusi.

Ujerumani nayo imezuia usafirishaji wa gesi kutoka Urusi kwa mifereji kupitia nchi hiyo hadi mataifa mengine ya Uropa. Urusi huzalisha asilimia 40 ya gesi ya kiasili duniani.

Taifa hilo pia ni la pili kwa uzalishaji mafuta ghafi kwa wingi duniani. Lak – ini vita vyake nchini Ukraine na vikwazo ilivyowekewa na mataifa ya kigeni vimevuruga usafirishaji wa bidhaa hi – yo, hali ambayo imepandisha bei yake katika masoko ya kimataifa.

Putin anapania kumwondoa mamlakani Rais Zelensky ambaye anamtuhumu kuwa kibaraka cha Amerika na mataifa 30 wanachama wa Kundi la kujihami la NATO.

  • Tags

You can share this post!

Mgogoro wa tiketi Azimio, raha kwa UDA

Kiini halisi cha wawaniaji kurukaruka

T L