• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Anaamini ana kipaji cha kufanya vizuri na kutinga upeo wa kimataifa

Anaamini ana kipaji cha kufanya vizuri na kutinga upeo wa kimataifa

Na JOHN KIMWERE

NDIYO ametinga miaka miwili tangia ajiunge na tasnia ya uigizaji lakini sura na jina lake sio geni kwa wapenzi wa vipindi vya maigizo hapa nchini.

Ni kati ya msanii anajivunia kuchota wafuasi wengi tu ambao hufuatilia kipindi cha Zora ambacho tangia mwaka uliyopita hupeperushwa kupitia Citizen TV.

Alice Mbeyu maarufu Zalena ni mwalimu mstaafu pia mwana mtindo wa mavazi kwa kipindi cha miaka kumi bila kuweka katika kaburi la sahau msanii wa matangazo ya kibiashara (Commercial Adverts).

”Kitaaluma nimekuwa mwalimu wa shule za upili ndani ya kipindi cha miaka 35 ambapo rasmi nilianza kushiriki uigizaji mwaka 2020,” alisema na kuongeza kuwa alivutiwa na tasnia ya maigizo akiwa shule ya Msingi. Hata hivyo tangia akiwa mtoto alidhamiria kuhitimu kuwa mhudumu wa ndege.

Alice Mbeyu maarufu Zalena kati ya waigizaji kwenye kipindi cha Zora…Picha/JOHN KIMWERE

NJORO WA UBA

Ameshiriki matangazo mengi ikiwamo tango Airtel, Velvex na KWFT kati ya mengine ambayo yamefanikiwa kupata mpenyo na kuonyeshwa kwenye runinga. Pia ameshiriki kipindi vya Real Talk na Tamima.

Katika uigizaji ndani ya miaka miwili ameshiriki vipindi kadhaa ikiwamo Varshita, Maria, Njoro wa Uba pia filamu fupi iitwayo Jaja. Msanii huyu aliyetua duniani mwaka 1966 anasema anamini ana kipaji cha kufanya vizuri na kutinga upeo wa kimataifa ndani ya miaka mitano ijayo.

”Katika mpango mzima nimepania kuwa kielelezo chema kwa vijana pia kina dada na wanawake kwa jumla. Pia nataka kuonyesha watu kuwa hakuna lililo gumu bora kujiamini na kuamini Mola,” akasema na kuongeza kuwa analenga kuonyesha jamii kuwa uzee sio ulemavu mradi kujituma na kutia bidii kwenye nyanja zozote. Kadhalika amepania kusaidia vijana kukuza talanta zao katika maigizo.

SERIKALI

Anadokeza kuwa inazidi kudhihirisha kuwa uigizaji una nafasi nzuri kutoa ajira kwa wasanii wengi wanaokuja wakubwa kwa wadogo. Kwa mtazamo huo anasema serikali inastahili kujenga vyuo vya masuala ya uigizaji katika zote 47 ili vijana wasomee taaluma hiyo. ”

Pia litakuwa jambo nzuri endapo shule za msingi zinaweza kutilia mkazo masuala ya uigizaji kwa wanafunzi wangali wadogo,” akasema na kuongeza kuwa kamwe wazazi hawapaswi kuwazuia wanao wanaojishughulisha na masuala ya usanii.

BEATIFULL SOUL

Katika mpango mzima anasema angependa sana kufanya kazi na wasanii wanaowika Afrika akiwamo Mercy Johnson (Nigeria) na Lupita Nyong’o (Kenya). Wawili hao wameshiriki filamu kama Beatifull Soul na Black Panther mtawalia.

Anashukuru wenzake waliotangulia kwa kuchangia ukuaji wa sekta hiyo hasa baadhi ya vituo vya runinga nchini kuanzisha vipindi vya burudani ya uigizaji. Anashukuru wakurungezi wa kampuni ya Fitty Pictures, Rashid Abdalla na Lulu Hassan kwa kumpa nafasi kuonyesha talanta yake katika uigizaji.

Fitty Pictures ndiyo iliyozalisha kipindi cha Maria season one ambapo season Two ipo njiani. Wawili hao ni katu ya watangazji wa kituo cha Citizen TV.

Alice Mbeyu maarufu Zalena kati ya waigizaji kwenye kipindi cha Zora….Picha/JOHN KIMWERE

You can share this post!

TAHARIRI: Jamii itajuta kuvumilia wahalifu walio kwa...

Boda boda watozwa faini ya Sh7Milioni

T L