• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Guardian Angel afanikisha ndoto ya kumiliki studio ya kulea chipukizi wa Injili

Guardian Angel afanikisha ndoto ya kumiliki studio ya kulea chipukizi wa Injili

NA FRIDAH OKACHI

MWANAMUZIKI Guardian Angel amezindua studio ya lebo ya Seven Heaven Musics almaarufu 7HM itakayotumiwa na vijana na wasanii chipukizi wa nyimbo za Injili.

Msanii huyo amemtaja mwanamziki anayetambulika kama DK Kwenye Beat kuwa ni mtu aliyemsaidia kurekodi wimbo, akiwa shule ya upili.

Amesema hayo katika mahojiano na Chipukeezy wakati wa uzinduzi huo.

“DK alinisaidia nikiwa Kidato cha Tatu. Nakumbuka alinipeleka studio na kulipia ili nirekodi muziki wangu wa kwanza,” akasema.

Guardian Angel anasema nia yake ni kusaidia vijana kufanikisha ndoto zao za muziki kama alivyosaidiwa na mwanamuziki DK Kwenye Beat.

“Sababu ya kuanzisha lebo mahususi ya muziki wa injili ni kufuta taswira ambayo watu walikuwa nayo kuhusiana na muziki wa injili,” akaongezea.

Mkewe Guardian Angel, Esther Musila vilevile amechapisha kwa ukurasa wa Instagram akiwashukuru wote waliofika kwenye uzinduzi huo kama vile msanii @chipukeezy@jaguarkenya na msimamizi wa studio hiyo @benjamin_otwal.

“Jamani naomba niwashukuru sana. Asante sana kwa ndugu na marafiki wangu, mashabiki, familia yangu, wachungaji, na wadau wa vyombo vyote vya habari ambao wamekuja kwenye uzinduzi huo. Nawashukuru zaidi. Ni wakati wa kutimiza ndoto kubwa,” alisema Bi Musila.

Mnamo Septemba 2023 Presenter Kai kwa pitapita zake, alimhoji Sammy G ambaye aliimba wimbo wake Guardian Angel na baadaye kutafutwa na msanii huyo.

Mnamo Oktoba 5, 2023, Guardian Angel alichapisha Remix ya kolabo na kutazamwa mara zaidi ya milioni 2.

Hatua hiyo ya kumhusisha Sammy G na wasanii wengine imefanya msanii huyo kupiga hatua kubwa na hata kupendwa zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Kituo cha afya cha Muteithania chafungwa kwa kuendesha...

KNEC yasema imezima mianya yote ya wizi wa mitihani ya KCPE...

T L