• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Jackie Matubia alipukia shabiki aliyemuuliza kiini cha kukosa hafla ya rafikiye Milly Chebby

Jackie Matubia alipukia shabiki aliyemuuliza kiini cha kukosa hafla ya rafikiye Milly Chebby

NA FRIDAH OKACHI

MWIGIZAJI Jackie Matubia amelipukia mashabiki wake waliojaribu kumkebehi kwa kukosa kuhudhuria sherehe ya harusi ya kitamaduni ya rafikiye Milly Chebby.

Matubia anafahamika kuwa rafiki wa karibu wa Chebby. Marafiki hao wamefanya mambo kwa pamoja hadi kuchapisha picha zao kwenye mitandao ya kijamii. Picha ya mwisho ilichapishwa kwenye kurasa zao mara ya mwisho ni Julai 4, 2023.

“Nina roho mbaya na sina bwana,” alijibu mwigizaji huyo baada ya shabiki mmoja kutaka kufahamu sababu ya kukosa hafla ya Chebby wikendi.

Mapema mwaka huu, mwigizaji huyo alimwambia Chebby kwa mahojiano ya moja kwa moja kwenye YouTube, kwanza hakupendezwa na uhusiano yao baada ya matukio kadhaa.

Mcheshi  Terence Creative na Milly Chebby  walifanikisha harusi ya kitamadumi baada ya kuishi pamoja kwa miaka 11.

Wawili hao walio na mtoto mmoja kike waliomba idhini ya kufunga ndoa rasmi kwa jamii ya Bi Chebby. Sherehe hiyo ikifahamika“Kuhoya Uhiki Chaike Ruracio.”

Kwenye ukurasa wake Instagram, Milly alimshukuru Maulana kwa kufanikisha sherehe hiyo.

“Endelea kujituma, ipo siku italeta maana yake. Mungu si mchoyo, anajibu maombi. Asante Mungu kunipa zawadi na kunijalia kupata mume,”aliandika Chebby.

Sherehe hiyo iliyofanyika katika Kaunti ya Nandi, ilihudhuriwa na familia, marafiki wa karibu; baadhi yao ikiwa ni wasanii na wanamuziki kama vile Bahati, Diana Marua, Jacky Vike, Flaqo, Keranta, MC Kajim, mcheshi Jemutai, Zeddy na Silva Kido.

Mwaka uliopita wapenzi hao wawili walijizawadi na gari aina ya Land Cruiser Prado TX kusherekea miaka kumi ya kuishi pamoja.

  • Tags

You can share this post!

Wito kaunti ijenge kituo cha utalii katika kijiji ambapo...

EACC yamtaka Mung’aro kusitisha mara moja zabuni ya...

T L