• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
Wito kaunti ijenge kituo cha utalii katika kijiji ambapo maji hupanda mlima

Wito kaunti ijenge kituo cha utalii katika kijiji ambapo maji hupanda mlima

NA SAMMY KIMATU

WENYEJI na wakazi wa Kaunti ya Machakos wameomba serikali ya kaunti ikiongozwa na Gavana Wavinya Ndeti kufufua mpango wa kujenga kituo cha utalii katika kijiji kya Kyamwilu.

Katika kijiji hicho, wakazi na wasafiri hujionea maajabu ya dunia ambapo maji hukaidi sayansi na badala ya kuteremka, huwa yanapanda mlima.

Wageni, wakiwemo wa kutoka kaunti nyingine ndani ya nchi, hufurika katika maeneo hayo mwishoni mwa juma kushuhudia makubwa hayo.

Akiongea na Taifa Leo mnamo Jumatatu, chifu wa eneo la Mutituni Bw Ancient Nzyoki alisema mwaka 2016, aliyekuwa waziri wa Utalii katika serikali ya aliyekuwa gavana wa Machakos, Bw Alfred Mutua, Bw Larry Wambua alizuru Kyamwilu akiongoza maafisa wengine kutoka Kaunti ya Machakos.

Aliongeza kwamba mapendekezo ya viongozi hao yalikuwa Kyamilu kujengwe kituo cha utalii ambapo serikali ya Machakos ingepata mapato huku nafasi za ajira kwa vijana kutoka eneo hilo zikibuniwa.

“Wakazi wa Kyamwilu walikuwa na matarajio makubwa wakitazamia kufaidika pakubwa ikiwa kituo cha utalii kitajengwa,” chifu Nzioki akasema.

Miaka minane baadaye, hakuna dalili ya mipango kuhusu ujenzi wa kituo hicho.

Sasa wakazi wanaomba serikali ya kaunti kufufua ndoto na kuitimiza kwa kujenga kituo hicho.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Teknolojia mpya ya CyberKnife tumaini la...

Jackie Matubia alipukia shabiki aliyemuuliza kiini cha...

T L