• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:26 PM
Mashabiki wasifu Wahu na Nameless kudumu pamoja licha ya hali tete ya ndoa za kisanii

Mashabiki wasifu Wahu na Nameless kudumu pamoja licha ya hali tete ya ndoa za kisanii

NA RICHARD MAOSI

WAKENYA mtandaoni wamepongeza Wahu na Nameless kwa kudumu ndani ya ndoa kwa miaka 18.

Hili likiwa ni funzo la karne na mfano mzuri wa kuigwa, miongoni mwa mastaa nguli, ambao wengi wao wameshindwa kusawazisha umaarufu na kudumisha uhusiano wa kimapenzi unaojikita kwa udhati wa moyo. Wengi wa mastaa katika tasnia ya burudani mara nyingi husaka kiki na kusahau umuhimu wa uaminifu katika ndoa.

Nameless ambaye alikutana na Wahu kwa mara ya kwanza wakiwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, amepakia ujumbe mzito wa kutia moyo, pale aliposifia safari yao kama yenye kumbukumbu tele.

“Leo tunasherehekea miaka 18 ya pingu za maisha kama mume na mke. Hakika tumeshuhudia kipindi cha furaha na wakati mwingine huzuni,” akasema.

Nameless anasema kwenye maisha miinuko na mabonde ni mambo ya kawaida ila wamejifunza kutanguliza maelewano na mapenzi ya kweli.

Ikiwa ni pamoja na kuzika tofauti zao kwenye kaburi la sahau na kuganga yajayo.

Nameless pia ametumia fursa hiyo kuwapa shavu mashabiki wake kwa kusimama naye kidete tangu anaanza kutoka kimuziki na kuonyesha walikuwa wakimheshimu Wahu.

Wahu na Nameless walijitosa kwenye muziki mwishoni mwa miaka ya tisini (1990s) na mwanzoni mwa 2000 wakitamba na vibao ‘Niangalie’ na ‘Megarider’ mtawalia.

  • Tags

You can share this post!

Dalili zote zaonyesha Eric Omondi amejitosa katika tope la...

Jinsi walinzi wa vigogo walivyochomoa bunduki na kurushiana...

T L