• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Mwanamuziki Muigai wa Njoroge akana ‘kumdhuru’ msanii Dennis Mutara

Mwanamuziki Muigai wa Njoroge akana ‘kumdhuru’ msanii Dennis Mutara

NA WANDERI KAMAU

UTATA unaomkumba mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili, Dennis Mutara, sasa umechukua mkondo mpya, baada ya baadhi ya wenyeji wa eneo la Kati kusema masaibu yake yamechangiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake.

Mjadala kuhusu masaibu ya mwanamuziki huyo yalizua mijadala mikali katika mitandao ya kijamii, baadhi ya watu wakimhusisha mwanamuziki wa injili Muigai wa Njoroge na changamoto anazopitia Bw Mutara.

Walidai kuwa Bw Njoroge ndiye aliyemwingiza Bw Mutara katika kundi la kitamaduni la jamii ya Agikuyu liitwalo “Gwata Ndai”, ambalo huendeleza tamaduni ya kuwatahiri wanawake.

Madai hayo yalieleza kuwa baada ya kuingizwa katika kundi hilo, Bw Mutara alivunja baadhi ya kanuni zake, hilo likiwa kiini cha masaibu yanayomwandama kwa sasa.

Lakini mnamo Jumanne, Septemba 12, 2023, Bw Njoroge alijitenga na madai hayo, akisema kwamba hajawahi kutangamana na Bw Mutara kwa muda wa zaidi ya miongo miwili, ambayo amekuwa kwenye tasnia ya muziki.

“Mimi sijawahi kutangamana na Bw Mutara. Nilitangamana naye mara moja tu, wakati nilimsaidia kurekodi video yake ya kwanza. Ndimi niliyempeleka kwenye studio. Tangu wakati huo, hatujawahi kuwa karibu tena. Mimi ni mwanamuziki aliyelelewa kanisani. Watoto wangu huwa wanaenda kanisani. Nina nyimbo zaidi ya 300, ninazoweza kuzitoa kwa miaka mingi ijayo. Ni vipi tena ninaweza kumdhuru mwanamuziki mwenzangu? Nawaomba wanaoeneza vumi hizo kukoma,” akasema Bw Njoroge, huku akionekana mwenye ghadhabu.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa kama watu wale wengine, “yuko tayari kujua kinachomsumbua Bw Mutara”.

“Mimi sijui kinachomsumbua Bw Mutara. Kama wengine, niko tayari kujua kiini cha masaibu yake, ikiwa ataamua kutueleza atakapoondoka hospitalini,” akasema Bw Njoroge.

Masaibu yanayomkumba mwanamuziki huyo yameibua mijadala mikali mitandaoni, kuhusu ikiwa baadhi ya wanamuziki wanatumia njia za giza kujipa umaarufu au kuwadhuru washindani wao.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti za Pwani zatakiwa kufunza vijana kuthamini wazee...

Simulizi ya bodaboda aliyeponea kifo mwenzake akifariki...

T L