• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Pasta atoa ushuhuda jinsi alivyoepuka kupata virusi vya Ukimwi licha ya uzinzi

Pasta atoa ushuhuda jinsi alivyoepuka kupata virusi vya Ukimwi licha ya uzinzi

NA FRIDAH OKACHI

MCHUNGAJI wa kanisa la Life Church International-Kiambu, Anthony Kahura Mwangi almaarufu ‘Pastor T Mwangi’ ametoa ushuhuda jinsi alivyoponea kuambukizwa virusi vya Ukimwi licha ya kushiriki mapenzi na wanawake wawili tofauti ambao waliaminika kuwa na zimwi hilo.

Pasta huyo alishangaa kupata hana virusi hivyo baada ya mwanamke wa kwanza kuzikwa na uvumi kuenea kuhusu sababu ya kifo chake. Aidha alisema yule wa pili naye ilisemekana alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume ambaye alizikwa kwa kuugua Ukimwi.

Matukio hayo yalitokea kabla ya pasta huyo kuokoka na kuachana na anasa za dunia.

“Ulikuwa ni wakati wa Krismasi, nilikuwa nimelewa na nikalala na mwanamke ambaye sikujua hali yake ya virusi vya Ukimwi. Wakati alipokufa tulimzika,” akasema kumhusu mwanamke wa kwanza.

Katika mkondo uo huo wa anasa, alianza kuchumbiana na mwanamke mwingine ambaye alikuwa ameambukizwa virusi na mwanamme mwingine. Haja ya mwanamke huyu kufanya mapenzi naye ilikuwa kulipiza kisasi kwa yale alipitia.

“Nilianza kuchumbiana na mwanamke mwingine na jambo kama hilo likajitokeza tena. Marafiki walinifahamisha mchumba huyo alikuwa ameabukizwa virusi na jibaba lililokuwa na ugonjwa huo. Hivyo basi alikuwa mgonjwa,” alisema.

Mchungaji huyo alishangazwa na matokeo ya vipimo vya ugonjwa huo. Cha kushangaza ni kuwa wakati alipoenda kufanya vipimo vya virusi vya Ukimwi alipatikana akiwa mzima kama kigongo, jambo analosema kuwa ni neema ya Mungu.

“Nilitembelea kituo cha kupima virusi na cha kushangaza sikupatikana na virusi hivyo. Ni Neema ya Mungu na Jinsi Bwana alivyonihifadhi mimi sijui,” alisema mchungaji huyo.

  • Tags

You can share this post!

Najuta sana kutounga Wanyonyi Ugavana Nairobi, Igathe...

Sibanduki, mke amkalia ngumu mumewe aliyetaka kumfurusha

T L