• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Sabina Chege: Kwa Pasta Ng’ang’a ndipo

Sabina Chege: Kwa Pasta Ng’ang’a ndipo

NA WANDERI KAMAU

MBUNGE Maalum Sabina Chege amesema kuwa alipata baraka zake kutoka kwa Kanisa la Neno Evangelism Centre, lake Pasta James Ng’ang’a.

Bi Chege, ambaye alikuwa amehudhuria harusi ya bintiye mhubiri huyo, Grace Neema Wanjiku,  mnamo Jumapili, alisema kuwa baraka zake alizitoa kwa ‘upako’ wa Pasta Ng’ang’a.

“Nilikuwa mshirika wa hili kanisa, na hapa ndipo nilipotoa baraka zangu,” akasema Bi Chege, ambaye ni Mbunge Maalum (Jubilee).

Akimpongeza Bi Wanjiku, Bi Chege alinukuu Biblia, katika Kitabu cha Mithali 18:22: “Anayempata mke huwa anapata baraka kutoka kwa Mungu), huku akiwapongeza wanandoa kwa harusi hiyo.

Akimjibu kiucheshi, Askofu Ng’ang’a alimrai Bi Chege kurejea katika kanisa hilo akiwa na Sh3 milioni.

“Wewe tuletee Sh3 milioni pekee. Sh1 milioni kati ya hizo zitakuwa za kutuomba radhi huku pesa zilizobaki zikiwa kama ada ya kurejea katika kanisa hili,” akasema Bw Ng’ang’a.

Bi Chege aliahidi kurudi pamoja na marafiki wake kushiriki ibada katika kanisa hilo. Aliwarai washirika wengine kuendelea kuiunga mkono.

“Mko katika mahali panapofaa. Katika madhabahu hii, mtapata neema za Mungu na atawafungulia milango,” akasema.

Bi Chege alianza safari yake ya kisiasa baada ya kuchaguliwa kama Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Murang’a mnamo 2013.

Aliibuka mshindi kwa kuzoa asilimia 96.6 ya kura.

Alichaguliwa tena mnamo 2017. Kwa sasa anahudumu kama Mbunge Maalum.

  • Tags

You can share this post!

Mauaji ya Sniper: Itumbi, Miguna waungana kushinikiza haki

‘Tunataka stima madhubuti 2024’

T L