• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
BORESHA AFYA: Mlo wako iwapo unanyonyesha

BORESHA AFYA: Mlo wako iwapo unanyonyesha

NA PAULINE ONGAJI

WATAALAM wa kiafya wanasema kwamba ili kuboresha afya ya mtoto, maziwa ya mama yanapaswa kuwa chakula chake cha kipekee kwa miezi sita ya kwanza maishani.

Hata hivyo, akina mama wengi hushindwa kutimiza sharti hili huku changamoto kuu ikiwa upungufu wa maziwa.

Kama mama anayenyonyesha, vyakula vifuatavyo vitakusaidia kuimarisha mtiririko wa maziwa:

  • Parachichi: Takriban asilimia 80 ya tunda hili ni mafuta ambayo humsaidia mama kusalia akiwa ameshiba. Pia, parachichi ni chanzo muhimu cha virutubisho vya vitamin B, vitamin K, vitamini C, vitamin E, folate na madini ya potassium.
  • Kokwa: Kokwa zina viwango vya juu vya madini kama vile chuma, calcium, na zinc, vile vile virutubisho kama vile vitamini K na B. Kando na hayo, kokwa pia zina viwango vya juu vya asidi zilizo na mafuta (essential fatty acids) na protini.
  • Maharagwe na nafaka zingine za jamii hii: Vyakula hivi vina viwango vya juu vya protini, vitamini na madini. Kulingana na wataalam, mbali na kuimarisha afya ya mama, kula aina tofauti za maharagwe katika kipindi cha kunyonyesha, kunaimarisha uzalishaji wa maziwa.
  • Uyoga: Aina nyingi za uyoga zinasemekana kuwa vyanzo murwa vya polysaccharide beta-glucan, homoni kuu katika uzalishaji maziwa.
  • Mboga: Mboga za kijani zina viwango vya juu vya phytoestrogens, viungo mfano wa homoni za estrogen, ambazo zimethibitishwa kuimarisha uzalishaji maziwa. Kwa upande mwingine, mboga nyekundu na za rangi ya chungwa kama vile karoti, kiazi kikuu na kiazi kitamu husaidia kuimarisha afya ya mama, vile vile kuchochea uzalishaji maziwa.
  • Bizari: Sifa za bidhaa hii kusaidia kukabiliana na uvimbeuchungu ni muhimu kwa afya ya mama na kuzuia vile vile kutibu maambukizi ya mastitis. Aidha, hutuliza ishara zinazohusishwa na tatizo la maziwa kuganda ndani ya matiti ya mama anayenyonyesha.
  • Tags

You can share this post!

PATA USHAURI WA DKT FLO: Kansa ya ulimi hujitokezaje?

MAKALA MAALUM: Kimojawapo cha vivutio 2023 ni ulainishaji...

T L