• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
PATA USHAURI WA DKT FLO: Kansa ya ulimi hujitokezaje?

PATA USHAURI WA DKT FLO: Kansa ya ulimi hujitokezaje?

Mpendwa Daktari,

Ningependa kujua mengi kuhusu ishara za kansa ya ulimi.

Jason, Mombasa

Mpendwa Jason,

Kansa ya ulimi hutokana na uvimbe unaoanza kujitokeza kwenye sehemu ya ulimi au nyuma ya koo.

Ishara za kansa ya ulimi

  • Sehemu fulani za ulimi kubadili rangi na kuwa nyekundu au nyeupe, huku sehemu hii ikiwa nyepesi na rahisi kuvuja damu.
  • Uchungu unapotafuna au meza kitu.
  • Kuchipuka kwa vidonda kwenye sehemu ya juu ya ulimi.
  • Maumivu ya koo ya kila mara
  • Kufa ganzi kwenye ulimi na mdomoni
  • Sauti kubadilika huku ulimi ukiwa mgumu na harufu mbaya mdomoni. Mgonjwa pia atahisi uchungu kila anapofungua mdomo.
  • Maumivu ya masikio
  • Uvimbe kwenye sehemu ya nyuma ya koo na uzani wa mwili kupungua kwa njia isiyo ya kawaida.

Masuala yanayoongeza hatari ya kukumbwa na kansa ya ulimi?

Matumizi ya tumbaku: Watu wanaotumia bidhaa za tumbaku kama vile sigara, wako katika hatari kubwa ya kukumbwa na maradhi haya.

Unywaji pombe: Pombe inasemekana kusababisha sio tu kansa ya ulimi bali pia aina zingine za kansa za mdomoni.

Kuwahi pitishwa kwenye miali ya mwanga: Iwapo uliwahi ugua aina ingine ya kansa kama vile ya kichwa au ya shingo, iliyokulazimu kupokea matibabu kwa miali ya mwanga, basi una uwezekano mkubwa wa kukumbwa na kansa ya mdomoni.

Kutozingatia lishe bora: Kutokula mboga na matunda kwa wingi, kunaongeza hatari ya kukumbwa na aina hii ya kansa.

Maambukizi ya virusi vya human papillomavirus HPV: Virusi hivi pia vimetambulika kama mojawapo ya vichocheo vya sio tu kansa ya mdomoni bali pia ya njia ya uzazi.

Unashauriwa kumuona daktari iwapo utashuhudia ishara za aina hii kwani aina hii ya kansa husambaa upesi katika sehemu zingine za mdomo kama vile ufizi, taya na koo.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Wadau kikaoni wahimiza hatua zaidi kupigwa...

BORESHA AFYA: Mlo wako iwapo unanyonyesha

T L