• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
BORESHA AFYA: Vitamini, madini na virutubisho bora vya kuimarisha mfumo wa kinga

BORESHA AFYA: Vitamini, madini na virutubisho bora vya kuimarisha mfumo wa kinga

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MFUMO wa kinga ni safu moja ngumu, yenye nguvu ya ulinzi inayolinda mwili dhidi ya vitu vya kigeni lakini ambavyo mwili umevisawiri kuwa hatari.

Ukikosa mfumo bora wa kingamwili, unaweza kusumbuliwa na maambukizo, mzio miongoni mwa matatizo mengine ya kiafya.

Habari njema ni kwamba mfumo wa kingamwili unaweza kuimarishwa.

Virutubisho vya kuimarisha mfumo wa kinga

Asidi ya folic

Asidi ya folic ni aina mojawapo ya folati ambayo ina vitamini B. Kwa kawaida ina jukumu muhimu kama mojawpo ya vyambajengo vya DNA na protini.

Vipande vya machungwa yaliyokatwa. PICHA | MARGARET MAINA

Upungufu mkubwa wa folati unaweza kuathiri vibaya mfumo wa kinga.

Vyakula vyenye folati ni mayai, mchicha, ini la ng’ombe, dengu, nafaka za kifungua kinywa, machungwa, kantalupi, na maharagwe.

Chuma

Chuma hujulikana sana kwa kutoa oksijeni kwa damu, ingawa madini hayo pia ni muhimu kwa kukuza mfumo mzuri wa kinga. Ulaji wa chakula chenye madini ya chuma nyingi hata hivyo unaweza kuongeza hatari ya maambukizo na athari nyingine mbaya za kiafya.

Kudumisha usawa wa chuma kunaweza kusaidia kusababisha kuleta usawazisho wa kawaida wa kinga katika mwili.

Baadhi ya vyakula vilivyo na madini ya chuma ni nyama ya ng’ombe, nyama ya ndege aina ya batamzinga, samaki, mboga za majani, kwinoa, soya, maharagwe, na dengu.

Vitamini A

Nyongeza ya vitamini A inaonyesha kuwa ya manufaa wakati mtu ana upungufu. Lakini ushahidi unaonyesha kuzidi viwango vya kawaida kunaweza kuwa na matokeo mabaya ya kiafya.

Vitamini kwa kiwango kilichopitiliza huzuia kinga ya mwili iliyozoeleka na hivyo kuongeza uwezekano wa kuambukizwa magonjwa tofauti.

Vyanzo vya vitamini A ni parachichi, karoti, boga, maembe, na papai miongoni mwa vyakula na matunda mengineyo.

Vitamini C

Vitamini C ndiyo inayojulikana zaidi “kichochezi cha mfumo wa kinga” kwa sababu kadhaa.

Vitamini C huchochea utengenezwaji wa seli nyeupe za damu, seli muhimu za kinga ambazo husaidia mwili kupigana na maambukizi.

Ulaji wa vitamini C mara kwa mara unaweza kupunguza muda wa maambukizo yanayohusiana na matatizo ya kupumua, pamoja na mafua makali.

Machungwa, mapera, tunda aina ya kiwi, pilipili mboga, na fyulusi ni vyanzo vizuri vya Vitamini C.

Vitamini E

Vitamini E ni muhimu katika kusaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu.

Kuongezewa na vitamini E kunaweza kudumisha mfumo wa kinga kwa kuathiri vyema mwitikio wa seli za kinga.

Vitamini E huwa kwenye vyakula kama lozi, karanga, mbegu za alizeti, mafuta ya mboga, mboga za majani, na nafaka za kiamsha kinywa zilizoimarishwa.

  • Tags

You can share this post!

Wakristo waonyesha undugu na Waislamu wakati wa Ramadhani

Vyakula vinavyoweza kuwasaidia walio na ugonjwa wa jongo...

T L