• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Changamoto zinazokumba baadhi ya lugha za Kiafrika

WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Changamoto zinazokumba baadhi ya lugha za Kiafrika

NA PROF JOHN KOBIA

WIKI hii (tarehe 24-30 Januari 2022) ni wiki ya lugha za Kiafrika.

Wiki ya lugha za Kiafrika ilitengwa na mataifa wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika kusherehekea mafanikio na umuhimu wa lugha za Kiafrika katika utambulisho, turathi na utamaduni.

Wiki hii inasherehekewa kwa mara ya kwanza mwaka huu kwa kaulimbiu, ‘Lugha za Kiafrika: Nyenzo za Afrika Tunayotaka’.

Kuna shughuli mbalimbali zilizoratibiwa kufanyika kote duniani wiki hii kusherehekea lugha za Kiafrika.

Mojawapo ya shughuli hizi ni kuandika makala kuhusu mafanikio na changamoto zinazokumbuka lugha za Kiafrika.

Kwa mfano lugha ya Kiswahili nchini Kenya imepiga hatua za maendeleo kimatumizi katika vyombo vya habari kama vile magazeti, redio na runinga.

Hata hivyo, kuna mafanikio kiasi ya lugha za Kiafrika katika mfumo wa elimu.

Licha ya hayo, lugha hizi zinakumbwa na changamoto tele.

Mtaala wa Umilisi unatambua lugha ya Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili inapaswa kufundishwa kuanzia Gredi ya Nne hadi ya Sita katika shule za msingi.

Mafunzo ya lugha ya Kiswahili yanatarajiwa kuendelea katika daraja ya awali ya shule ya upili kutoka Gredi ya Saba hadi ya Tisa.

Isitoshe, somo la lugha ya Kiswahili lipo katika Gredi ya Kumi hadi ya Kumi na Mbili.

Ingawa mtaala unatambua lugha ya Kiswahili, somo hili ni la hiari.

Hivyo basi, huwepo uwezekano wa wanafunzi wengi kuacha somo la lugha ya Kiswahili na kukimbilia masomo mengine yanayofikiriwa kuwa yana nafasi bora zaidi ya ajira.

MAKALA YATAENDELEA…

  • Tags

You can share this post!

WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Tuadhimishe wiki hii ya lugha za...

Hii hapa siri ya jinsi ya kujiandaa vyema kupita mtihani...

T L