• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 8:50 AM
WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Tuadhimishe wiki hii ya lugha za Kiafrika kwa kuhimiza matumizi fasaha ya Kiswahili

WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Tuadhimishe wiki hii ya lugha za Kiafrika kwa kuhimiza matumizi fasaha ya Kiswahili

Na WALLAH BIN WALLAH

WIKI hii ni ya maadhimisho ya lugha za Kiafrika kwa mujibu wa wito na tangazo rasmi la makao makuu ya Nchi za Umoja wa Afrika.

Awali ya yote, naomba kuwapongeza wapenzi wa Kiswahili; walimu, wanafunzi, wasomaji, wazungumzaji, waandishi na watangazaji wa lugha ya Kiswahili kwa kuchangia makuzi na maenezi ya Kiswahili humu nchini na ulimwenguni kote!

Lugha ya Kiswahili imekua na kuzidi kupiga hatua kubwa zaidi!

Wakuzaji ni sisi wazungumzaji na watumiaji!

Hivyo basi, tunapoadhimisha wiki hii ya lugha za Kiafrika, tukishehenezee Kiswahili hadhi stahiki kwa matumizi bora, sahihi na fasaha kila tunapokitumia popote tulipo!

Mazoea na mazoezi ya kutumia lugha kwa usahihi ndizo nyenzo halisi za kujijengea ufasaha!

Heri mtu ayatumie maneno machache tu ya Kiswahili kila wakati lakini kwa uhakika na ufasaha kuliko kuyabwabwaja maneno mengi shaghalabaghala yaliyokusanya makosa na matumizi yasiyofuata kanuni safi za lugha ya Kiswahili!

Licha ya lugha ya Kiswahili kukumbukwa na vikwazo vingi vya wapinzani wanaodhani Kiswahili ni lugha duni, tushukuru hakuna awezaye kufunika jua kwa ungo wala kuyazuia maji ya mto kutiririka kuelekea baharini!

Ndugu wapenzi, tuadhimishe wiki ya lugha za Kiafrika kwa kusoma vitabu na magazeti ya Kiswahili kama vile Taifa Leo na mengineyo kila siku ili tujiongezee maarifa na ufasaha kamili!!

Kiswahili oyeeee!!!!!!!

  • Tags

You can share this post!

WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Ukoloni ulivyochangia tabia ya...

WIKI YA LUGHA ZA KIAFRIKA: Changamoto zinazokumba baadhi ya...

T L