• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 2:49 PM
DINI: Kunyamaza kwa Mungu si ishara hakupendi

DINI: Kunyamaza kwa Mungu si ishara hakupendi

NA MHUBIRI PADRE WYCLIFFE OTIENO

LABDA uko katika hali ngumu na umejaribu kila njia na huoni matumaini.

Kuna wakati unamwomba Mungu na ni kama hayuko. Unajaribu maombi na kufunga, unatoa hata sadaka lakini mambo hayabadiliki. Unasoma Biblia, unaenda kanisani, lakini Mungu bado yuko kimya.

Kuna wakati unatamani tu hata upate ishara kuwa Mungu amekusikia, lakini wapi? Mambo yanawezakwenda vibaya, kila kitu kinaweza kubadilika maishani mpaka ufike katika kiwango cha kushuku kama kweli Mungu yupo.

Kwa hakika kuna wakati Mungu hunyamaza. Kuna wakati maombi yanaonekana kutojibiwa. Lakini kunyamaza kwa Mungu si kutokuweko kwake.

Kunyamaza kwa Mungu sio ishara kuwa hakupendi. Kunyamaza kwake sio lazima iwe ni ishara kuwa umetenda dhambi.

Watu wengi hujihukumu na kusononeka mno wanapopitia katika hali kama hiyo. Lakini usikate tamaa unapoona mambo yanaenda usivyotarajia na ni kama Mungu hashughuliki.

Ukweli wa Mambo ni kuwa Mungu anajali na anashughulika. Twahitaji kuwa na moyo kama wa Daudi aliyesema kwa Zaburi 23, “Bwana ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.”

Katika msitari wa 4 anasema, “Naam, nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami.”

Wakati mwingine Mungu anaweza kunyamaza ili akushughulikie. Labda Mungu anakuandaa kwa mambo makubwa. Labda kimya chake kinanuia kujenga subira ndani yako. Wakati mwingine kimya chake kinasusha kiburi chako. Biblia yasema katika 1 Yohana 2:16, “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.”

Mungu akinyamaza, jiangalie mwenyewe. Usilalamike, mruhusu Mungu akuandae. Fanya bidii kujiboresha katika kila eneo la maisha yako. Baada ya Yusufu kuota ndoto jinsi atakavyokuwa mkubwa katika familia yao, hakusikia tena sauti ya Mungu.

Alipitia mateso mengi sana. Aliuzwa na nduguze, aliwekelewa mambo ya uongo na mkewe Potifa, alitupwa gerezani, lakini Mungu bado alikuwa naye.

Ingawaje Mungu alikuwa kimya, kuna kazi alikuwa anafanya katika maisha yake. Wakati unaofaa ulipofika, alimwinua Yusufu akawa waziri mkuu wa Misri

  • Tags

You can share this post!

Wito serikali isambaze chakula kwa wakazi wa Ganze na Bamba

Wanachama KKA wavutania viti serikalini

T L