• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
DOMO: Kwa sasa yuko freshi barida!

DOMO: Kwa sasa yuko freshi barida!

NA MWANAMIPASHO

MWANZO kabisa hivi mumeyaskia mapya kutoka Purity Vishinewa a.k.a Pritty ambaye ni Ex wake Stivo Simple Boy?

Baada ya kuachana na msela, Pritty kaoga na kurudi soko na sasa anasema kuwa yeyote anayetaka kumchumbia, ni lazima awe tayari kumlipia mahari ya Sh2 milioni.

Huh! Kama hela za Uganda ni sawa na kama ni za Tanzania, basi ni afadhali ila kama ni za Kanairo, mimi simo. Hivi ni shamba nitanunua au mwana nitahangaika kupeleka hela ndefu ukweni. Halafu tukiachana iwe nimeingia hasara mara mbili? Haiwezekani! Sifanyi biashara hiyo ya kishamba. Sio katika maisha haya, au yajayo. Biashara mahesabu, kwa hili hamna hesabu kabisa.

Halafu nikiwa hapo kwenye mada ya mahari, nimekumbuka kitu. Ila wengine wenu wachokozi ajabu.

Hivi aliyemwambia Pritty anafanana na marehemu Rais Mwai Kibaki ni nani haswa? Nilimwona akicharuka kweli. Mlimtia hasira kwa ufananisho huo. Pritty haamini kabisa, duniani kuna wawili wawili. Yaani kufanana kupo. Ila hii sio mada niliyokuwa nawazia sema zinahusiana. Acha nigeuze upepo sasa.

Kusema kweli nimeipenda menejimenti mpya ya Stivo Simple Boy aka ‘Ndo Maanake’.

Ukweli wa mambo ni kwamba tunamfuatilia Stivo kwa ajili ya kupata burudani. Sio kwamba sisi ni mashabiki wakubwa wa sanaa yake ila tunafuatilia kuona kipi cha kutufurahisha. Kikweli anatufurahisha ukianza na mwonekano wake. Mwenyewe anajua, kajaliwa maumbile ya kuchekesha kwani kumtizama tu, kicheko kinakuja.

Halafu sasa ongeza na zile voko za kwake, aisee, ametosha kukuvunja mbavu ukaumwa na tumbo mwezi mzima.

Ni sifa hizi ndizo zimempa umaarufu na ndio sababu tunamfuatilia na kumsapoti. Ukweli ni kuwa kama yupo makini, huu ndio wakati anahitaji kutumia fursa zilizopo kujinyooshea maisha. Tumewashuhudia mastaa kibao walioshindwa kutumia fursa zao vyema wakija baadaye kutuitisha michango. Siwezi kupenda hili limtokee Stivo kusema kweli. Mimi bwana ananichangamsha kinoma.

Kwa kutojua, umaarufu ulipomkuta alijikuta na menejimenti iliyoamua kumnyonya pasi na kumhurumia maisha ya uchochole anayotokea.

Pritty aliwahi fichua kuwa menejimenti yake ya zamani ilikuwa inamnyonya. Kwa mfano kuna shoo alipiga na kulipwa Sh120,000, fedha hizo zilipitishwa kwa menejimenti, alicholipwa Stivo ni Sh4,000. Menejimenti hiyo aidha ilikuwa ndio inadhibiti akaunti zake za benki na chaneli za mitandao ya kijamii na YouTube.

Vyanzo vyote hivi vya uchumi, menejimenti hiyo ilikuwa ikifaidi. Hata makazi ilimkodishia Kayole baada ya kumhamisha kutoka Kibera, sehemu ambayo hakuweza kushawishiwa aachane nayo.

Mwisho wa siku alitoka huko na sasa ana menejimenti mpya. Mpaka sasa wameonyesha nia njema na Stivo. Baada ya kauli yake Freshi Barida kuwa maarufu, wamefanya hima na kuisajilisha kama hakimiliki ya Stivo. Huwezi sasa kutumia kauli hiyo kwa matangazo yoyote ya kibiashara bila baraka zake. Lakini pia nimeona amezindua ‘hoods’ zake za Freshi Barida.

Ni maombi yangu nao hawa hawatafika sehemu wamgeuke dogo nao waanze kumkamua. Ila kwa sasa, wako freshi barida.

  • Tags

You can share this post!

Zetech Sparks yapania kumaliza tatu-bora KWPL

KIKOLEZO: Riri, huyo Kanairo

T L