• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Ezekiel Odero aonya watu dhidi ya kusherehekea siku maalum ya kuzaliwa    

Ezekiel Odero aonya watu dhidi ya kusherehekea siku maalum ya kuzaliwa   

NA MERCY KOSKEI

PASTA Ezekiel Odero mwanzilishi wa Kanisa la New Life Prayer Centre ameonya watu dhidi ya kusherehekea siku zao za kuzaliwa, ikiwa hawajatimiza hatua muhimu maishani.

Mhuribiri Odero anadai kwamba siku za kuzaliwa zinapaswa kuadhimishwa wakati mtu ametimiza jambo la maana.

Pasta Odero anaamini kuwa siku ya kuzaliwa inapaswa kuadhimishwa tu wakati watu wana mafanikio yanayoonekana.

Katika video inayosambaa mitandaoni, iliyonaswa wakati wa mahubiri katika kanisa lake, Ezekiel alisema kuwa siku ya kuzaliwa inafaa kuonyesha mafanikio ya mtu badala ya tambiko la kila mwaka.

“Usisherehekee siku yako ya kuzaliwa ikiwa hujafanya lolote. Subiri hadi upate kitu, ndipo tunaweza kusherehekea siku hiyo maalum,” Mchungaji Odero alisema.

Alifichua kwamba hajawahi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, na aliapa kutofanya hivyo katika maisha yake yote.

Badala yake, alisema kuwa anaamini kwamba kizazi kijacho kitamsherehekea atakapoaga dunia, mradi tu ataishi maisha ya maana sana.

Pasta huyo alitoa ulinganifu wa sherehe za kuzaliwa na kufa kwa Yesu Kristo.

“Ndio maana tunasherehekea kuzaliwa na kifo cha Yesu Kristo. Umewahi kunisikia nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa? Hutanisikia. Watakaokuja nyuma yangu ndio watakaoamua kama niliishi maisha yenye thamani kubwa. Kusherehekea au la, hakuna askari anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa sababu yuko nyikani na kuna vita vya kweli,” aliendelea kueleza.

Mhubiri huyo mwenye Kanisa katika Kaunti ya Kilifi aidha alitilia shaka mila ya wachungaji kusherehekea siku zao za kuzaliwa, akishangaa wanapata wapi nyakati za sherehe hizo.

“Huwa najiuliza, wachungaji hupata wapi muda wa kusherehekea siku zao za kuzaliwa?” aliuliza.

  • Tags

You can share this post!

Ruto aahidi wakulima wa miwa minofu, akisisitiza msimamo...

Biashara za uchuuzi wa dawa za mende na panya mitaani...

T L