• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Fahamu mengi kuhusu nyama ya sungura

Fahamu mengi kuhusu nyama ya sungura

Na MARGARET MAINA

[email protected]

SUNGURA ni mnyama ambaye faida ziambatanazo na ufugaji wake ni nyingi.

Nyama ya sungura ina protini nyingi na mafuta kidogo ikilinganishwa na nyama ya kondoo na kadhalika. Kwa hiyo, nyama ya sungura ni nzuri kuliwa na watu ambao wana magonjwa mbalimbali.

Ina protini nyingi

Nyama ya sungura huongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha protini ambayo ni asilimia 21 ikifatiwa na ile ya kuku yenye asilimia 18.

Mpaka sasa hakuna nyama yenye kiwango kuzidi hiki. Ulaji wa nyama ya sungura unakupa protini nyingi zaidi kuliko nyama nyingine yoyote ambayo unaweza kuipata.

Ina kiwango kidogo cha lehemu

Kwa kutumia nyama ya sungura unakuwa unaepuka madhara hayo kwa kiwango kikubwa.

Ina kiwango kidogo cha sodiamu hivyo ni nyama bora kwa ajili ya watu wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo

Nyama ya sungura ni nyeupe. Nyama nyekundu huwa na Nucleic aside nyingi ambazo huchangia Uric acid nyingi ambayo katika mwili wa mlaji inatakiwa ikae katika hali ya kumiminika na mwili ukishindwa au kuzidiwa hizi asidi hutengeneza chembe chembe za maungio (joints) na kusababisha maumivu (gout). Pia nyama nyekundu huwa na lipoprotein ambayo huchochea utengenezaji wa lehemu yenye madhara. Kwa kula nyama ya sungura, haya yote yanaepukika.

Haina mafuta mengi

Na ina mafuta ambayo hayana madhara mwilini mwa mtumiaji.

TANBIHI

Baadhi ya watu hawali nyama ya sungura kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafundisho ya kidini.

You can share this post!

Mzozo wa mpaka eneo la Maseno walipuka upya

CECIL ODONGO: Kauli ya Kalonzo na Mudavadi ithibati hawana...

T L