• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Faida za mboga aina ya karela (bitter gourd)

Faida za mboga aina ya karela (bitter gourd)

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KARELA ni aina mojawapo ya mboga zenye afya. Imejaa antioxidants, vitamini na madini. Inaweza kuliwa kama mboga, kachumbari au kutayarishwa kama juisi.

Kuna faida nyingi za matumizi ya mara kwa mara ya karela.

Karela ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari

Karela ina bidhaa inayofanya kazi sawa na insulini. Inapunguza viwango vya sukari ya damu. Kunywa glasi ya juisi ya karela ni hatua nzuri sana hivi kwamba wagonjwa wa kisukari wanahitaji mara kwa mara. Inaweza pia kusaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari cha ujauzito.

Je, kisukari cha ujauzito ni nini? Ni aina ya kisukari ambayo hugunduliwa kwa mara ya kwanza kwa wajawazito ambao hawakuwa na kisukari kabla ya kuwa wajawazito.

Nzuri kwa ngozi na nywele

Karela ina wingi wa antioxidants na vitamini A na C ambazo ni nzuri kwa ngozi. Husaidia katika kupunguza kuzeeka na kupambana na chunusi na madoa kwenye ngozi.

Ni muhimu katika kutibu magonjwa mbalimbali. Juisi ya karela huongeza mng’ao kwa nywele na hupambana na mba, tatizo la nywele kukatika na migawanyiko hafifu ya nywele.

Kisafishaji cha ini

Karela husaidia kusafisha ini na huondoa sumu. Huongeza vimeng’enya kwenye ini na ni tiba nzuri kwani inapunguza amana za pombe kwenye ini. Kibofu cha mkojo na utumbo pia hunufaika kwa kutumia karela.

Ni nzuri kwa usagaji chakula

Karela imejaa nyuzi na husaidia kuboresha choo. Huondoa kuvimbiwa na huipa tumbo utulivu.

Inaboresha afya ya moyo

Karela hupunguza lehemu mbaya na kupunguza hatari ya kupata mshtuko wa moyo. Nyuzinyuzi zilizo kwenye karela pia husaidia kufungua mishipa.

Kupunguza uzito

Karela husaidia kupunguza uzito kwani ina kalori chache na ina nyuzinyuzi nyingi. Inazuia malezi na ukuaji wa seli ambazo huhifadhi mafuta mwilini. Inaboresha mfumo wa kimetaboliki, na ina antioxidants zinazosaidia kuondoa sumu mwilini na kusababisha kupungua kwa mafuta.

  • Tags

You can share this post!

Umuhimu wa kula vitamini mara kwa mara

Karim Benzema anyakua taji la Ballon d’Or kwa mara ya...

T L