• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Genge linaloiba mifugo Murang’a na kuacha kinyesi cha binadamu katika boma

Genge linaloiba mifugo Murang’a na kuacha kinyesi cha binadamu katika boma

Na MWANGI MUIRURI

GENGE la uhalifu linalovamia maboma ya watu Murang’a na kuiba mifugo, kisha kuacha limekunia katika boma limeibuka.

Genge hilo limeibua wasiwasi miongoni mwa wenyeji, wakililia serikali kuweka mikakati maalum kulinga mifugo wao.

Katika kisa cha hivi karibuni, genge hilo limevamia Kijiji cha Gaitegi kilichoko eneobunge la Kiharu.

Baada ya kuiba mifugo usiku wa manane, kila memba ndani ya genge hilo huwa anajisaidia haja kubwa katika boma kama ishara ya nguvu na pia kutokuwa na haraka.

“Mimi niliamkia wizi wa mbuzi wangu wawili wa maziwa mnamo Juni 14, 2023. Lakini kilinichoshangaza ni kwamba kulikuwa na milima midogo mitano ya kinyesi cha watu wazima na hapo ndipo nilibashiri kwamba nilivamiwa na genge la wasiopungua watano,” akasema Bw James Njogu.

Katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, kijiji hiki kimekuwa kikivamiwa mara kwa mara na ng’ombe, mbuzi, kuku, nguruwe na pia sungura kuibwa.

Visa sawa na hivo vimesambaa katika kaunti nzima ambapo imekuwa vigumu sana kwa wakulima kuwekeza katika sekta ya ufugaji.

“Hii ni hujuma kubwa kwa uchumi wa mashinani kwa kuwa hatuwezi tukafuga wanyama ili tujikimu kimaisha. Wezi hawa wamesambaratisha kwa kiwango kikuu uwekezaji katika sekta za maziwa, mayai na nyama,” akasema mwenyekiti wa muungano wa wafugaji wa kiwango cha chini Bw Phillip Kariuki.

Tayari, Kamishna wa Kaunti ya Murang’a Bw Patrick Mukuria ametoa amri kwa kamati za kiusalama katika wadi zote 35 wawajibikie hatari za wezi wa mifugo na wale wa mavuno.

“Tunajua kwamba magenge haya yanasaka pesa za kugharamia uraibu wa ulevi na mihadarati. Nimeagiza magenge hayo yaandamwe kwa ushirika wa raia na vitengo vya kiusalama,” akasema.

 

[email protected]

 

 

  • Tags

You can share this post!

Karen Nyamu anunulia Samidoh pombe ya bei ghali...

Akothee awakemea wanaodai mumewe mzungu ‘amesota’  

T L