• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Hamasisho kuhusu uhifadhi wa mikoko

Hamasisho kuhusu uhifadhi wa mikoko

Na ALEX KALAMA

SERIKALI ya kitaifa na ya kaunti ya Kilifi imetakiwa kuhamasisha umma kuhusu mikopo ya kaboni kwa wale wanaohusika na uhifadhi wa mikoko.

Lengo la mpango huu ni kuboresha uchumi wa eneo hilo na kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.

Mwanzilishi wa Gro with us, Paul Flynn, anaamini kuwa kutekeleza mikakati sahihi ya kuhamasisha ufahamu wa mikopo ya kaboni kutasaidia kujenga imani kati ya jamii za kimataifa.

Ni kutokana na hilo, afisa huyo anahimiza serikali ya kitaifa na ya kaunti ya Kilifi kukuza faida za mikopo ya kaboni kwani inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa jamii na kuvutia wawekezaji wa kimataifa.

“Ninaisihi serikali kuu na ile ya kaunti ya Kilifi kuanza kutetea manufaa ya mikopo ya kaboni. Kwa sababu ikifanywa vyema inakuwa chanzo cha mapato kwa jamii na pia kwa kuvutia wawekezaji wa kimataifa,” asema Bw Flynn.

Mkurugenzi Mtendaji wa Gro with us Afrika, Kelly Banda, anaeleza kuwa lengo lao ni kurejesha upangaji wa mikoko Kaunti ya Kilifi, kulingana na Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG) na ajenda ya Rais William Ruto ya mwaka 2030 ya kuongeza asilimia 10 ya miti ya misitu.

Dkt Ruto ameweka shabaha mpya, kutinga asilimia 30 kufikia 2032.

“Ikiwa mpango huu utakubaliwa na kufanywa kwa nia njema Kilifi itakuwa ikizalisha maelifu ya tani za kaboni kila mwaka, huko kwa kupata mapato na kuunda fursa kubwa ya kuunganisha watu wa ndani na jumuiya ya kimataifa,” asema.


Paul Flynn Mwanzilishi Gro With Us wakati wa mahojiano Kilifi. Picha / ALEX KALAMA

Shirika hilo tayari limepanda zaidi ya mimea milioni 2.5 ya mikoko huko Kidundu na Watamu, Kaunti ya Kilifi.

Misitu ya mikoko inajulikana kwa ufanisi wake katika kukamata kaboni, wakati gesi nyingi hukusanywa kwenye udongo badala ya kuwa kwenye mimea.

Kukata ovyo miti ya mikoko kwa ajili ya mbao na makaa ya mawe kumekuwa tishio kubwa kwa mazingira, hasa Kilifi, ambapo wakazi wanategemea miti hiyo kwa ajili ya maisha yao.

“Tunafanya mpango huu sambamba na serikali na pia kujaribu kusaidia jamii katika masuala ya riziki. Utunzaji wa mizinga ya nyuki na mabwawa ya samaki ili hali ya kiuchumi ya wenyeji ibadilike na kuwa na maisha bora,” Band aliambia Taifa Leo Dijitali kupitia mahojiano ya kipekee.

Walakini, ikiwa wenyeji watapewa elimu kuhusu faida za mikopo ya kaboni, inaaminika kuwa tishio hili linaweza kupunguzwa.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Mtongani-Kidundu Self Help, Stephen Chivatsi, anahimiza serikali kutenga bajeti zaidi na kuja na sera bora ambazo zitaimarisha uhifadhi wa mikoko na kuwawezesha jamii.

  • Tags

You can share this post!

Vyakula vinavyoweza kuwasaidia walio na ugonjwa wa jongo...

Kocha apongeza wachezaji Thika Queens ikisaka ubingwa Kombe...

T L