• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Hawa Wanyamwezi ni mibabe, wakulima na waastarabu mno

Hawa Wanyamwezi ni mibabe, wakulima na waastarabu mno

Na HAWA ALI

WANYAMWEZI ni moja ya makabila ya Waswahili linalopatikana nchini Tanzania mkoani Tabora.

Tabora ndio mkoa mkubwa zaidi nchini Tanzania. Kabila hili lina historia ndefu sana; lina zaidi ya miaka 500. Ni kabila la kibantu lenye koo nyingi kutoka sehemu mbalimbali.Neno Wanyamwezi mwanzoni lilitumiwa tu kama sehemu ya kutambua koo mbalimbali za Kiafrika.

Na lina maana ya watu wa Mwezini. Yaani sehemu ambayo mwezi huchomoza.Jina hili walilipata kutokana na kufanya biashara na watu wa Pwani ambapo wakati huo kulikuwa na maeneo ya kibiashara kama Kilwa na Bagamoyo.

Kuna maeneo ya utawala yaliyokuwepo katika kabila hili la Wanyamwezi. Inasimuliwa kuwa kulikuwa na maeneo tawala 31, ambayo kila moja lilikuwa na utawala wake na lilikuwa linajitegemea.

Katika kabila la Wanyamwezi kuna mashina (makabila matano) ambayo yanafanana kitabia, asili, lugha, desturi n.k. Mashina hayo ni kabila la Wanyamwezi, Wakonongo, Wakimbu, Wasumbwa na Wasukuma.

Kabila linaloongoza kwa watu wengi ni Wasukuma wakifuatwa na Wanyamwezi. Ndilo kabila linaongooza kwa ushujaa na mapambano, ndio maana viongozi wao ni maarufu zaidi kuliko wa makabila mengine. Ina maana kuwa hakukuwa na chifu mmoja aliyewahi kutawala kabila la Wanyamwezi.

Utawala

Licha ya kwamba kulikuwa na utofauti kati ya maeneo ya utawala, bado haikumaanisha kuwa eneo moja la kiutawala lilikuwa bora zaidi ya jingine. Kimsingi kila eneo tawala lilikuwa na namna yake ya kipekee ya kujiendesha.

Ni kweli kulikuwa na watawala ambao walikuwa na nguvu sana na wababe, kama wakina Chifu Mirambo (Milambo), Kapela na Fundikira. Lakini bado watemi hao hawakuwahi kutawala kabila la Wanyamwezi.

Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Ulyankuru, Ugunda, Kiwere, Uyowa, Busagari, Unyanyembe, Ngulu, Karunde, Ibili, Bukumbi, Mwakaru na kadhalika.Wanyamwezi wanasifika kwa kilimo na ufugaji pia kwa ukarimu wa hali ya juu.

Kuna dhana kwamba Mnyamwezi ni mtu yeyote yule mwema miongoni mwa vijana, kama vile kijana anayejua kuvaa vizuri, asiyependa kufuatilia mambo ya watu wengine na anayeweza kuwafahamisha wenziwe na kuwafanya waelewe juu ya jambo fulani.

You can share this post!

Kaunti yasaidia wakazi kukata rufaa ya ardhi

Wajumbe wa Ford-K Bungoma waapa kuchagua Wetangula tena

T L