• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Wajumbe wa Ford-K Bungoma waapa kuchagua Wetangula tena

Wajumbe wa Ford-K Bungoma waapa kuchagua Wetangula tena

Na BRIAN OJAMAA

MAAFISA wa Ford Kenya katika Kaunti ya Bungoma wamesema kuwa watamchagua Seneta wao Moses Wetang’ula kama kiongozi wa chama hicho.

Chama hicho kitaandaa Kongamano Kuu la Wajumbe Novemba 4 katika ukumbi wa Bomas ambao viongozi wapya wanatarajiwa kuchaguliwa. Hadi sasa hakuna mwanasiasa yeyote ambaye ametangaza kuwa atampinga Bw Wetang’ula wakati wa kura hiyo.

“Hadi sasa hakuna mwaniaji yeyote ambaye amelipa Sh1 milioni zinazohitajika kuwania wadhifa wa kiongozi wa chama mbali na Bw Wetang’ula,” akasema Mwakilishi wa Kike wa Bungoma, Catherine Wambilianga.

Hata hivyo, mrengo wa waasi wa Ford Kenya wakiongozwa na wabunge Wafula Wamunyinyi (Kanduyi) na Dkt Eseli Simiyu (Tongaren) walisema Kongamano la Wajumbe (NDC) linalotambulika ni lao, na litaandaliwa Novemba 6 katika ukumbi wa Kasarani.

“Baada ya kongamano la Bomas hakuna mwanachama yeyote ambaye ataruhusiwa kuhudhuria jingine tofauti,” akasema Bw Wambilianga.

Kiongozi wa wengi wa Bunge la Kaunti ya Bungoma Joseph Nyongesa naye ametaka mrengo wa Dkt Eseli na Bw Wamunyinyi wanafaa wahudhurie kongamano la Bomas kama njia ya kumaliza uhasama ambao umezingira Ford Kenya kwa muda wa mwaka moja uliopita.

You can share this post!

Hawa Wanyamwezi ni mibabe, wakulima na waastarabu mno

Gavana abuni jopokazi kuchunguza madai hatari kuhusu visa...

T L