• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Hayawi hayawi…Jackie Matubia afichua mchumba wake mpya   

Hayawi hayawi…Jackie Matubia afichua mchumba wake mpya  

NA FRIDAH OKACHI

MWIGIZAJI Jackie Matubia amemtambulisha kwa umma mpenzi wake mpya, siku chache tu baada ya kudokeza kwamba ana nia kutaka kuolewa.

Ijumaa, Desemba 8, 2023 mama huyo wa watoto wawili alipakia video zake Instagram na Facebook akiwa kwenye bwawa la kuogelea na mwanamume ambaye hakufichua majina yake.

Katika video hizo, wapenzi hao wawili walionekana wamejawa na furaha wakiwa pamoja.

“Jinsi tunavyotulia tukisubiri tukio letu lijalo,” aliandika.

Katika video nyingine, wawili hao walionekana wakiogelea kwenye bwawa huku kipenzi chake cha roho akimbusu mashavuni.

Matubia alificha sehemu ya uso wa mwanamume wake mpya kwa picha za mapenzi.

Aidha, video alizopakia kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram aliziambatanisha na na wimbo wa mapenzi unaofahamika Perfect Design.

Mwezi Julai 2023, mama huyo wa watoto wawili alitengana na mume wake, Blessing Lungaho ambaye wamejaaliwa mtoto mmoja naye.

Bi Matubia alishangaza mashabiki wake akisema anafurahia kuwa mzazi wa pekee kwa wanawe wawili.

Novemba 2023, muigizaji huyo alizidiwa na hisia wakati akisimulia jinsi amefanikiwa kulea wanawe wawili bila usaidizi wa baba zao.

Kupitia chaneli yake ya You-Tube alizungumzia kwa undani kilichomfanya kuondoka katika uhusiano wake.

 

  • Tags

You can share this post!

Kindiki atakiwa kutuliza uhalifu Pokot Magharibi

Mzozo wa DPP na IPOA kuhusu askari watundu

T L