• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:50 AM
JIJUE DADA: Lishe bora, usingizi mwanana ni njia bora ya kutunza ngozi yako

JIJUE DADA: Lishe bora, usingizi mwanana ni njia bora ya kutunza ngozi yako

NA PAULINE ONGAJI

HAKUNA atakaye kuzeeka mapema maishani.

Hata hivyo, hii ni awamu isiyoepukika maishani. Mojawapo ya sehemu zinazoanza kuonyesha kutimia kwa kipindi hiki ni ngozi, na ndiposa unashauriwa kuishughulikia vilivyo.

Kushughulikia ngozi kunahusisha kudumisha lishe bora kwa kula mboga pamoja na matunda kwa wingi na kunywa maji zaidi ya lita 1.5, kupata usingizi wa kutosha, kufanya mazoezi, kujiepusha na matumizi ya tumbaku na unywaji pombe kupindukia.

Pia unashauriwa kunawa uso asubuhi na jioni ukitumia maji, kutumia sunscreen, kulinda ngozi yako kutokana na miale ya jua na kujiepusha na matumizi ya bidhaa kali za ngozi.

Ikiwa una wasiwasi wowote kuhusiana na ngozi yako, tafadhali muone mtaalamu wa ngozi.

Kuhusiana na vipodozi, pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa bidhaa hizi.

Hata hivyo, kuna baadhi ya mabadiliko ya ngozi ambayo hayawezi rekebishwa ila pengine kupitia upasuaji wa kurekebisha viungo (plastic surgery).

  • Tags

You can share this post!

MUME KIGONGO: Mwanamume atunze afya kupata mbegu bora ya...

MAKALA MAALUM: Kwa nini tuktuk ni kipenzi cha wengi Mombasa

T L