• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
JIJUE DADA: Nini husababisha kina dada kupoteza hamu ya tendo la ndoa?

JIJUE DADA: Nini husababisha kina dada kupoteza hamu ya tendo la ndoa?

NA PAULINE ONGAJI

KUNA baadhi ya wanawake ambao wakati mmoja maishani watakumbwa na tatizo la kupungukiwa au kupoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa.

Shida hii yaweza sababishwa na masuala ya kimwili, kisaikolojia, kijamii au yote.

Baadhi ya vichocheo

•Matayarisho duni kabla tendo la ndoa kwa upande wa mwanamume. Shughuli hii huhusisha kuamsha ashiki za mwanamke kabla kushiriki ngono.

•Aliyopitia mtu hapo awali. Hofu ya kushiriki tendo la ndoa yaweza tokana na shida alizokumbana nazo mtu, kama kudhulumiwa kimapenzi au uhusiano wa hapo awali unaomfanya kuhusisha tendo la ndoa na uchungu au maumivu.

•Matumizi ya baadhi ya dawa za kupanga uzazi au za kudhibiti msongo wa akili.

•Shida za kimwili na hasa sehemu za kike na mfumo wa mkojo kama vile endometriosis, cystitis, ukavu katika sehemu ya uke au maradhi ya vaginitis. Maradhi kama hypothyroidism, kisukari, multiple sclerosis, pia huathiri hamu ya mwanamke ya tendo la ndoa.

•Kuondolewa kwa uterasi au matiti kwa upasuaji kutokana na sababu za kiafya, pia kwaweza athiri mwanamke kisaikolojia na hivyo kumpunguzia ashiki wakati wa kushiriki ngono.

•Matumizi ya baadhi ya dawa kwa wingi, dawa za kulevya au kunywa pombe kupindukia.

•Umri pia huathiri hamu ya mwanamke kutaka kufanya mapenzi. Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wengi wanapokaribia au kufikisha umri wa miaka 60, hupoteza hamu. Kulingana na utafiti huo, ni asilimia 15 pekee ya wanawake wanaozidi kuwa na hamu hii baada ya kukatikiwa.

Ishara za kupungukiwa na hamu ya kushiriki ngono

•Kukosa ashiki kabla tendo la ndoa.

•Kukosa raha wakati wa tendo la ndoa na badala yake kukumbwa na maumivu.

•Kutokuwa na fikra za kuongeza ashiki.

You can share this post!

Junet, Babu wadadisiwa na DCI

GWIJI WA WIKI: Baraka Phil

T L