• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Jinsi mateka wa bangi alivyofyeka familia ya watu nane nusura awaangamize

Jinsi mateka wa bangi alivyofyeka familia ya watu nane nusura awaangamize

NA MWANGI MUIRURI

WATU wanane wa familia moja katika Kaunti ya Murang’a, akiwemo ajuza wa miaka 78, waliponea kifo baada ya kushambuliwa na jamaa wao mraibu wa mihadarati mnamo Machi 14 mwaka huu.

Akifunguka hivi majuzi, Bw Francis Maina asema aligundua mwanawe wa kiume wa kipekee Eric Mwangi, 20, alikuwa akitumia dawa za kulevya miaka mitano iliyopita baada ya kuacha shule akiwa Darasa la Nane.

“Juhudi zetu za kumshauri aache mienendo hiyo mibaya zilikosa kuzaa matunda. Baadaye alipandwa na hasira za kiajabu kiasi kwamba nusra atuangamize sote wanane katika familia yetu,” akasema.

Kisa hicho kilitokea katika kijiji cha Kamataathi eneobunge la Kiharu mwendo wa saa nne za asubuhi.

“Nilimwona ndugu yangu akiingia ndani ya shamba la ndizi ambako huvutia bangi na kumeza vidonge vya dawa ya kulevya aina ya benzodiazepine,” anasimulia Catherine Wairimu, 18.

Kakake alikuwa hapo kwa dakika 10 kisha akaanza kupiga mayowe akiapa kumuua yeyote atakayemwona.

“Haikunishtua kwani nilijua hawezi kufanya kitu kama hicho. Kadhalika, hakuonyesha dalili zozote za kutekeleza mauaji,” alisema Bi Wairimu.

Lakini siku hiyo Bw Mwangi aliingia katika chumba chake kabla kutoka bila shati huku ameshika panga mkononi, na kumrukia dadake.

“Niliogopa sana. Nilisimama tu ni kama nimeganda kama sanamu. Nilimwona kwa karibu … sikupiga kelele. Mkono wake wa kulia ulishikilia panga huku akipiga mayowe,” Bi Wairimu anaeleza.

Binti huyo alirusha mkono wake wa kulia na mara akahisi maumivu makali kwenye kifundo na upande wa kushoto wa shingo yake.

“Maumivu yalinifanya nipige kelele huku nikitokwa damu. Niliamua kukimbia niokoe maisha yangu huku kakangu akinifuata kwa mayowe,” aliongeza.

Binamu zake watatu – wanaume wawili na mwanamke – pamoja na baba yake walimwona akikimbia huku akifuatwa unyounyo na nduguye.

Wote walifanikiwa kuruka ndani ya ghala na kujifungia kutoka ndani huku wakipiga kelele.

Tukio hilo lilivuta nyanyake Mwangi, Bi Naomi Wangari, ambaye alikuwa kwake jikoni akiandaa chakula cha mchana.

“Nilisikia kelele nikatoka nje kuangalia ni nini ndipo nikakutana na Mwangi. Nilimwita na akanikodolea macho mekundu. Alikuwa amepagawa. Alinishambulia mimi pia nikaanza kupiga mayowe,” Bi Wangari, 78, aliambia Taifa Leo.

Kijana huyo alimshambulia nyanyake na kumkata kichwa.

Tukio hilo pia ilivuta makini ya mjombake Bw Mwangi, Herman Irungu, 48, ambaye alikuwa nyumbani kwake.

“Nilimpata mama yangu akiwa amepoteza ufahamu huku akivuja damu kichwani. Wakati huo, Mwangi alikuwa akipiga mayowe huku akisema kuwa anakabiliana na maadui,” akasema Bw Irungu.

“Alianza kunishambulia pia ila nikajiokoa kw akumpiga teke. Badaa ya hapo, nikaanza kupiga mayowe na majirani wakakuja.”
Wanakjiji waliokasirishwa na tukio hilo walimshambulia Mwangi na kumuuwa papo hapo.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Kwanza: Ruto asema ‘form’ ni kubembeleza...

Nimesikia fununu kwamba huyu chali akilamba...

T L