• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Jinsi ya kuandaa maharagwe

Jinsi ya kuandaa maharagwe

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • maharagwe kilo nusu
  • tui kikombe 1
  • kitunguu saumu kilichotwangwa kijiko 1
  • kitunguu maji kilichokatwa
  • pilipili mboga iliyokatwa
  • karoti iliyoparwa
  • chumvi
  • mafuta ya kupikia
  • Royco kijiko 1
  • nyanya 3 zilizosagwa
  • maji ya kuchemshia kiasi

Maelekezo

Safisha maharagwe kwa kuondoa uchafu wote na yaoshe vizuri. Weka kwenye sufuria kisha mimina maji.

Funika sufuria kisha chemsha maharagwe mpaka maji yatakapopungua.

Ongeza maji mengine na uache yachemke mpaka yapungue.

Sasa weka maji kidogo kidogo yasifunike maharagwe yako ili yaive bila ya kutoka magamba.

Endelea kuongeza maji kidogo kidogo mpaka yaive.

Kwenye sufuria tofauti, weka mafuta na uache yapate moto.

Weka vitunguu maji uvikaange huku ukiwa makini uhakikishe haviungui.

Ongeza pilipili mboga na ukaange vizuri.

Weka karoti huku ukiendelea kukaanga. Mwisho, weka kitunguu saumu huku ukiendelea kukaanga.

Sasa mimina nyanya zilizosagwa kisha koroga mchanganyiko wako

Weka chumvi na Royco kisha funika na uache vichemke kwa dakika moja.

Mimina maharagwe uyaache kwa dakika moja kisha mimina tui acha lichemke kwa dakika tatu.

Epua halafu subiri kwa muda wa dakika tano ndipo upakue.

Unaweza kula na wali, ugali au slesi za mkate.

You can share this post!

Juventus wakomoa Zenit na kuingia 16-bora UEFA

Kocha Unai Emery aongoza Villarreal kupiga Young Boys...

T L